Selected
Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani
Abdullah Yusuf Ali
Abdul Majid Daryabadi
Abul Ala Maududi
Ahmed Ali
Ahmed Raza Khan
A. J. Arberry
Ali Quli Qarai
Hasan al-Fatih Qaribullah and Ahmad Darwish
Mohammad Habib Shakir
Mohammed Marmaduke William Pickthall
Muhammad Sarwar
Muhammad Taqi-ud-Din al-Hilali and Muhammad Muhsin Khan
Safi-ur-Rahman al-Mubarakpuri
Saheeh International
Talal Itani
Transliteration
Wahiduddin Khan
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.
71:1
إِنَّآ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِۦٓ أَنْ أَنذِرْ قَوْمَكَ مِن قَبْلِ أَن يَأْتِيَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
71:1
Hakika Sisi tulimtuma Nuh'u kwa watu wake: Uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:2
قَالَ يَـٰقَوْمِ إِنِّى لَكُمْ نَذِيرٌ مُّبِينٌ
71:2
Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhaahiri kwenu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:3
أَنِ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ وَٱتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ
71:3
Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye, na mumt'ii. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:4
يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرْكُمْ إِلَىٰٓ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ إِنَّ أَجَلَ ٱللَّهِ إِذَا جَآءَ لَا يُؤَخَّرُ ۖ لَوْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ
71:4
Atakughufirieni madhambi yenu, na atakuakhirisheni mpaka muda ulio wekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapo fika haucheleweshwi. Laiti mngejua! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:5
قَالَ رَبِّ إِنِّى دَعَوْتُ قَوْمِى لَيْلًا وَنَهَارًا
71:5
Akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu usiku na mchana, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:6
فَلَمْ يَزِدْهُمْ دُعَآءِىٓ إِلَّا فِرَارًا
71:6
Lakini wito wangu haukuwazidisha ila kukimbia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:7
وَإِنِّى كُلَّمَا دَعَوْتُهُمْ لِتَغْفِرَ لَهُمْ جَعَلُوٓا۟ أَصَـٰبِعَهُمْ فِىٓ ءَاذَانِهِمْ وَٱسْتَغْشَوْا۟ ثِيَابَهُمْ وَأَصَرُّوا۟ وَٱسْتَكْبَرُوا۟ ٱسْتِكْبَارًا
71:7
Na hakika mimi kila nilipo waita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakatakabari vikubwa mno! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:8
ثُمَّ إِنِّى دَعَوْتُهُمْ جِهَارًا
71:8
Tena niliwaita kwa uwazi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:9
ثُمَّ إِنِّىٓ أَعْلَنتُ لَهُمْ وَأَسْرَرْتُ لَهُمْ إِسْرَارًا
71:9
Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:10
فَقُلْتُ ٱسْتَغْفِرُوا۟ رَبَّكُمْ إِنَّهُۥ كَانَ غَفَّارًا
71:10
Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:11
يُرْسِلِ ٱلسَّمَآءَ عَلَيْكُم مِّدْرَارًا
71:11
Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:12
وَيُمْدِدْكُم بِأَمْوَٰلٍ وَبَنِينَ وَيَجْعَل لَّكُمْ جَنَّـٰتٍ وَيَجْعَل لَّكُمْ أَنْهَـٰرًا
71:12
Na atakupeni mali na wana, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:13
مَّا لَكُمْ لَا تَرْجُونَ لِلَّهِ وَقَارًا
71:13
Mna nini hamweki heshima ya Mwenyezi Mungu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:14
وَقَدْ خَلَقَكُمْ أَطْوَارًا
71:14
Na hali Yeye kakuumbeni daraja baada ya daraja? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:15
أَلَمْ تَرَوْا۟ كَيْفَ خَلَقَ ٱللَّهُ سَبْعَ سَمَـٰوَٰتٍ طِبَاقًا
71:15
Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba kwa matabaka? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:16
وَجَعَلَ ٱلْقَمَرَ فِيهِنَّ نُورًا وَجَعَلَ ٱلشَّمْسَ سِرَاجًا
71:16
Na akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:17
وَٱللَّهُ أَنۢبَتَكُم مِّنَ ٱلْأَرْضِ نَبَاتًا
71:17
Na Mwenyezi Mungu amekuotesheni katika ardhi kama mimea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:18
ثُمَّ يُعِيدُكُمْ فِيهَا وَيُخْرِجُكُمْ إِخْرَاجًا
71:18
Kisha atakurudsheni humo na atakutoeni tena. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:19
وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُمُ ٱلْأَرْضَ بِسَاطًا
71:19
Na Mwenyezi Mungu amekukunjulieni ardhi kama busati. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:20
لِّتَسْلُكُوا۟ مِنْهَا سُبُلًا فِجَاجًا
71:20
Ili mtembee humo katika njia zilizo pana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:21
قَالَ نُوحٌ رَّبِّ إِنَّهُمْ عَصَوْنِى وَٱتَّبَعُوا۟ مَن لَّمْ يَزِدْهُ مَالُهُۥ وَوَلَدُهُۥٓ إِلَّا خَسَارًا
71:21
Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika hao wameniasi, na wamemfuata yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila khasara. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:22
وَمَكَرُوا۟ مَكْرًا كُبَّارًا
71:22
Na wakapanga vitimbi vikubwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:23
وَقَالُوا۟ لَا تَذَرُنَّ ءَالِهَتَكُمْ وَلَا تَذَرُنَّ وَدًّا وَلَا سُوَاعًا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسْرًا
71:23
Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa' wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:24
وَقَدْ أَضَلُّوا۟ كَثِيرًا ۖ وَلَا تَزِدِ ٱلظَّـٰلِمِينَ إِلَّا ضَلَـٰلًا
71:24
Na hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:25
مِّمَّا خَطِيٓـَٔـٰتِهِمْ أُغْرِقُوا۟ فَأُدْخِلُوا۟ نَارًا فَلَمْ يَجِدُوا۟ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ أَنصَارًا
71:25
Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni, wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:26
وَقَالَ نُوحٌ رَّبِّ لَا تَذَرْ عَلَى ٱلْأَرْضِ مِنَ ٱلْكَـٰفِرِينَ دَيَّارًا
71:26
Na Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:27
إِنَّكَ إِن تَذَرْهُمْ يُضِلُّوا۟ عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوٓا۟ إِلَّا فَاجِرًا كَفَّارًا
71:27
Hakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)
71:28
رَّبِّ ٱغْفِرْ لِى وَلِوَٰلِدَىَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيْتِىَ مُؤْمِنًا وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَـٰتِ وَلَا تَزِدِ ٱلظَّـٰلِمِينَ إِلَّا تَبَارًۢا
71:28
Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliye ingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)