Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

15 Al-Ĥijr ٱلْحِجْر

< Previous   99 Āyah   The Rocky Tract      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

15:1 الٓر ۚ تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱلْكِتَـٰبِ وَقُرْءَانٍ مُّبِينٍ
15:1 Alif Lam Ra. (A. L. R). Hizi ni Aya za Kitabu na Qur'ani inayo bainisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:2 رُّبَمَا يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَوْ كَانُوا۟ مُسْلِمِينَ
15:2 HUENDA ikawa walio kufuru wakatamani wange kuwa Waislamu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:3 ذَرْهُمْ يَأْكُلُوا۟ وَيَتَمَتَّعُوا۟ وَيُلْهِهِمُ ٱلْأَمَلُ ۖ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
15:3 Waache wale, na wastarehe, na iwazuge tamaa. Watakuja jua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:4 وَمَآ أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلَّا وَلَهَا كِتَابٌ مَّعْلُومٌ
15:4 Na hatukuuangamiza mji wowote ule ila ulikuwa na muda wake maalumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:5 مَّا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَـْٔخِرُونَ
15:5 Hawawezi watu wowote kuitangulia ajali yao, wala kuchelewa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:6 وَقَالُوا۟ يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِى نُزِّلَ عَلَيْهِ ٱلذِّكْرُ إِنَّكَ لَمَجْنُونٌ
15:6 Na walisema: Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:7 لَّوْ مَا تَأْتِينَا بِٱلْمَلَـٰٓئِكَةِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
15:7 Mbona hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:8 مَا نُنَزِّلُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ إِلَّا بِٱلْحَقِّ وَمَا كَانُوٓا۟ إِذًا مُّنظَرِينَ
15:8 Sisi hatuwateremshi Malaika ila kwa sababu ya haki, na hapo hawatapewa muhula. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:9 إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا ٱلذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُۥ لَحَـٰفِظُونَ
15:9 Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:10 وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ فِى شِيَعِ ٱلْأَوَّلِينَ
15:10 Na hakika tulikwisha watumia Mitume mataifa ya mwanzo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:11 وَمَا يَأْتِيهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ
15:11 Na hakuwafikia Mtume ila walimkejeli. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:12 كَذَٰلِكَ نَسْلُكُهُۥ فِى قُلُوبِ ٱلْمُجْرِمِينَ
15:12 Na kama hivi ndivyo tunavyo ingiza katika nyoyo za wakosefu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:13 لَا يُؤْمِنُونَ بِهِۦ ۖ وَقَدْ خَلَتْ سُنَّةُ ٱلْأَوَّلِينَ
15:13 Hawayaamini haya, na hali ya kuwa umekwisha wapitia mfano wa watu wa kale. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:14 وَلَوْ فَتَحْنَا عَلَيْهِم بَابًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فَظَلُّوا۟ فِيهِ يَعْرُجُونَ
15:14 Na lau tungeli wafungulia mlango wa mbingu, wakawa wanapanda, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:15 لَقَالُوٓا۟ إِنَّمَا سُكِّرَتْ أَبْصَـٰرُنَا بَلْ نَحْنُ قَوْمٌ مَّسْحُورُونَ
15:15 Basi wangeli sema: Macho yetu yamelevywa, bali sisi wenyewe tumerogwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:16 وَلَقَدْ جَعَلْنَا فِى ٱلسَّمَآءِ بُرُوجًا وَزَيَّنَّـٰهَا لِلنَّـٰظِرِينَ
15:16 Na hakika tumeweka katika mbingu vituo vya sayari, na tumezipamba kwa wenye kuangalia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:17 وَحَفِظْنَـٰهَا مِن كُلِّ شَيْطَـٰنٍ رَّجِيمٍ
15:17 Na tumezilinda na kila shetani afukuzwaye. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:18 إِلَّا مَنِ ٱسْتَرَقَ ٱلسَّمْعَ فَأَتْبَعَهُۥ شِهَابٌ مُّبِينٌ
15:18 Isipo kuwa mwenye kusikiliza kwa kuibia, naye hufuatwa na kijinga cha moto kinacho onekana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:19 وَٱلْأَرْضَ مَدَدْنَـٰهَا وَأَلْقَيْنَا فِيهَا رَوَٰسِىَ وَأَنۢبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ شَىْءٍ مَّوْزُونٍ
15:19 Na ardhi tumeitandaza na humo tumeweka milima, na tumeotesha kila kitu kwa kiasi chake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:20 وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَـٰيِشَ وَمَن لَّسْتُمْ لَهُۥ بِرَٰزِقِينَ
15:20 Na tumekujaalieni humo vitu vya maisha yenu, na ya hao ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:21 وَإِن مِّن شَىْءٍ إِلَّا عِندَنَا خَزَآئِنُهُۥ وَمَا نُنَزِّلُهُۥٓ إِلَّا بِقَدَرٍ مَّعْلُومٍ
15:21 Na hakuna chochote ila asili yake inatokana na Sisi; wala hatukiteremshi ila kwa kipimo maalumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:22 وَأَرْسَلْنَا ٱلرِّيَـٰحَ لَوَٰقِحَ فَأَنزَلْنَا مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءً فَأَسْقَيْنَـٰكُمُوهُ وَمَآ أَنتُمْ لَهُۥ بِخَـٰزِنِينَ
15:22 Na tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka mbinguni maji, kisha tukakunywesheni maji hayo. Wala si nyinyi mnayo yaweka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:23 وَإِنَّا لَنَحْنُ نُحْىِۦ وَنُمِيتُ وَنَحْنُ ٱلْوَٰرِثُونَ
15:23 Na Sisi ndio tunao huisha na tunao fisha. Na Sisi ndio Warithi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:24 وَلَقَدْ عَلِمْنَا ٱلْمُسْتَقْدِمِينَ مِنكُمْ وَلَقَدْ عَلِمْنَا ٱلْمُسْتَـْٔخِرِينَ
15:24 Na tunawajua walio tangulia katika nyinyi, na tunawajua walio taakhari. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:25 وَإِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَحْشُرُهُمْ ۚ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمٌ
15:25 Na hakika Mola wako Mlezi ndiye atakaye wakusanya. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mjuzi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:26 وَلَقَدْ خَلَقْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ مِن صَلْصَـٰلٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
15:26 Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:27 وَٱلْجَآنَّ خَلَقْنَـٰهُ مِن قَبْلُ مِن نَّارِ ٱلسَّمُومِ
15:27 Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:28 وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَـٰٓئِكَةِ إِنِّى خَـٰلِقٌۢ بَشَرًا مِّن صَلْصَـٰلٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
15:28 Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa sura. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:29 فَإِذَا سَوَّيْتُهُۥ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِن رُّوحِى فَقَعُوا۟ لَهُۥ سَـٰجِدِينَ
15:29 Basi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu, basi mumwangukie kumsujudia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:30 فَسَجَدَ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ كُلُّهُمْ أَجْمَعُونَ
15:30 Basi Malaika wote pamoja walimsujudia, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:31 إِلَّآ إِبْلِيسَ أَبَىٰٓ أَن يَكُونَ مَعَ ٱلسَّـٰجِدِينَ
15:31 Isipo kuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na walio sujudu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:32 قَالَ يَـٰٓإِبْلِيسُ مَا لَكَ أَلَّا تَكُونَ مَعَ ٱلسَّـٰجِدِينَ
15:32 (Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata hukuwa pamoja na walio sujudu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:33 قَالَ لَمْ أَكُن لِّأَسْجُدَ لِبَشَرٍ خَلَقْتَهُۥ مِن صَلْصَـٰلٍ مِّنْ حَمَإٍ مَّسْنُونٍ
15:33 Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliye muumba kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yenye sura. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:34 قَالَ فَٱخْرُجْ مِنْهَا فَإِنَّكَ رَجِيمٌ
15:34 (Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika wewe ni maluuni! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:35 وَإِنَّ عَلَيْكَ ٱللَّعْنَةَ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلدِّينِ
15:35 Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:36 قَالَ رَبِّ فَأَنظِرْنِىٓ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ
15:36 Akasema (Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka siku watapo fufuliwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:37 قَالَ فَإِنَّكَ مِنَ ٱلْمُنظَرِينَ
15:37 (Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika walio pewa muhula - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:38 إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْوَقْتِ ٱلْمَعْلُومِ
15:38 Mpaka siku ya wakati maalumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:39 قَالَ رَبِّ بِمَآ أَغْوَيْتَنِى لَأُزَيِّنَنَّ لَهُمْ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ
15:39 Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:40 إِلَّا عِبَادَكَ مِنْهُمُ ٱلْمُخْلَصِينَ
15:40 Ila waja wako walio safika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:41 قَالَ هَـٰذَا صِرَٰطٌ عَلَىَّ مُسْتَقِيمٌ
15:41 Akasema: Hii Njia ya kujia kwangu Iliyo Nyooka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:42 إِنَّ عِبَادِى لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَـٰنٌ إِلَّا مَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلْغَاوِينَ
15:42 Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao, isipo kuwa wale wapotofu walio kufuata. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:43 وَإِنَّ جَهَنَّمَ لَمَوْعِدُهُمْ أَجْمَعِينَ
15:43 Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipo ahidiwa wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:44 لَهَا سَبْعَةُ أَبْوَٰبٍ لِّكُلِّ بَابٍ مِّنْهُمْ جُزْءٌ مَّقْسُومٌ
15:44 Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:45 إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّـٰتٍ وَعُيُونٍ
15:45 Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:46 ٱدْخُلُوهَا بِسَلَـٰمٍ ءَامِنِينَ
15:46 (Wataambiwa:) Ingieni kwa salama na amani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:47 وَنَزَعْنَا مَا فِى صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ إِخْوَٰنًا عَلَىٰ سُرُرٍ مُّتَقَـٰبِلِينَ
15:47 Na tutaondoa chuki iliyo kuwamo vifuani mwao, wawe ndugu juu ya viti vya enzi wameelekeana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:48 لَا يَمَسُّهُمْ فِيهَا نَصَبٌ وَمَا هُم مِّنْهَا بِمُخْرَجِينَ
15:48 Humo hayatawagusa machofu, wala hawatatolewa humo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:49 ۞ نَبِّئْ عِبَادِىٓ أَنِّىٓ أَنَا ٱلْغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ
15:49 Waambie waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:50 وَأَنَّ عَذَابِى هُوَ ٱلْعَذَابُ ٱلْأَلِيمُ
15:50 Na kwamba adhabu yangu ndio adhabu iliyo chungu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:51 وَنَبِّئْهُمْ عَن ضَيْفِ إِبْرَٰهِيمَ
15:51 Na uwape khabari za wageni wa Ibrahim. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:52 إِذْ دَخَلُوا۟ عَلَيْهِ فَقَالُوا۟ سَلَـٰمًا قَالَ إِنَّا مِنكُمْ وَجِلُونَ
15:52 Walipo ingia kwake na wakasema: Salama! Yeye akasema: Hakika sisi tunakuogopeni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:53 قَالُوا۟ لَا تَوْجَلْ إِنَّا نُبَشِّرُكَ بِغُلَـٰمٍ عَلِيمٍ
15:53 Wakasema: Usiogope. Sisi tunakubashiria kijana mwenye ujuzi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:54 قَالَ أَبَشَّرْتُمُونِى عَلَىٰٓ أَن مَّسَّنِىَ ٱلْكِبَرُ فَبِمَ تُبَشِّرُونَ
15:54 Akasema: Mnanibashiria nami uzee umenishika! Basi kwa njia gani mnanibashiria? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:55 قَالُوا۟ بَشَّرْنَـٰكَ بِٱلْحَقِّ فَلَا تَكُن مِّنَ ٱلْقَـٰنِطِينَ
15:55 Wakasema: Tunakubashiria kwa haki; basi usiwe miongoni mwa wanao kata tamaa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:56 قَالَ وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِۦٓ إِلَّا ٱلضَّآلُّونَ
15:56 Akasema: Na nani anaye kata tamaa na rehema ya Mola wake Mlezi ila wale walio potea? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:57 قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا ٱلْمُرْسَلُونَ
15:57 Akasema: Hebu nini amri yenu, enyi wajumbe? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:58 قَالُوٓا۟ إِنَّآ أُرْسِلْنَآ إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ
15:58 Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya wakosefu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:59 إِلَّآ ءَالَ لُوطٍ إِنَّا لَمُنَجُّوهُمْ أَجْمَعِينَ
15:59 Isipo kuwa walio mfuata Luut'i. Bila ya shaka sisi tutawaokoa hao wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:60 إِلَّا ٱمْرَأَتَهُۥ قَدَّرْنَآ ۙ إِنَّهَا لَمِنَ ٱلْغَـٰبِرِينَ
15:60 Ila mkewe. Tunakadiria huyo atakuwa miongoni watao bakia nyuma. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:61 فَلَمَّا جَآءَ ءَالَ لُوطٍ ٱلْمُرْسَلُونَ
15:61 Basi wale wajumbe walipo fika kwa Luut'i, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:62 قَالَ إِنَّكُمْ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ
15:62 Alisema (Luut'i): Hakika nyinyi ni watu msio juulikana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:63 قَالُوا۟ بَلْ جِئْنَـٰكَ بِمَا كَانُوا۟ فِيهِ يَمْتَرُونَ
15:63 Wakasema: Bali sisi tumekuletea yale waliyo kuwa wakiyafanyia shaka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:64 وَأَتَيْنَـٰكَ بِٱلْحَقِّ وَإِنَّا لَصَـٰدِقُونَ
15:64 Na tumefika kwako kwa Haki, na hakika sisi tunasema kweli. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:65 فَأَسْرِ بِأَهْلِكَ بِقِطْعٍ مِّنَ ٱلَّيْلِ وَٱتَّبِعْ أَدْبَـٰرَهُمْ وَلَا يَلْتَفِتْ مِنكُمْ أَحَدٌ وَٱمْضُوا۟ حَيْثُ تُؤْمَرُونَ
15:65 Basi ondoka na ahli zako usiku ungalipo, nawe ufuate nyuma yao, wala yeyote kati yenu asigeuke nyuma. Na mwende mnapo amrishwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:66 وَقَضَيْنَآ إِلَيْهِ ذَٰلِكَ ٱلْأَمْرَ أَنَّ دَابِرَ هَـٰٓؤُلَآءِ مَقْطُوعٌ مُّصْبِحِينَ
15:66 Na tukamfunulia hukumu hiyo, ya kwamba hata wa mwisho wao hao ikifika asubuhi atakuwa kesha katiliwa mbali. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:67 وَجَآءَ أَهْلُ ٱلْمَدِينَةِ يَسْتَبْشِرُونَ
15:67 Na wakaja watu wa mji ule nao furahani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:68 قَالَ إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ ضَيْفِى فَلَا تَفْضَحُونِ
15:68 Akasema: Hakika hawa wageni wangu, basi msinifedheheshe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:69 وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَلَا تُخْزُونِ
15:69 Na mcheni Mwenyezi Mungu, wala msinihizi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:70 قَالُوٓا۟ أَوَلَمْ نَنْهَكَ عَنِ ٱلْعَـٰلَمِينَ
15:70 Wakasema: Sisi hatukukukataza usimkaribishe yeyote? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:71 قَالَ هَـٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِىٓ إِن كُنتُمْ فَـٰعِلِينَ
15:71 Akasema: Hawa binti zangu, ikiwa nyinyi ni watendaji. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:72 لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِى سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ
15:72 Naapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:73 فَأَخَذَتْهُمُ ٱلصَّيْحَةُ مُشْرِقِينَ
15:73 Ukelele ukawatwaa wakipambaukiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:74 فَجَعَلْنَا عَـٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن سِجِّيلٍ
15:74 Na tukaigeuza nchi juu chini, na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo wa Motoni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:75 إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّلْمُتَوَسِّمِينَ
15:75 Hakika katika hayo zipo ishara kwa waaguzi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:76 وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلٍ مُّقِيمٍ
15:76 Na miji hii ipo kwenye njia inayo pitiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:77 إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً لِّلْمُؤْمِنِينَ
15:77 Hakika katika hayo ipo ishara kwa Waumini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:78 وَإِن كَانَ أَصْحَـٰبُ ٱلْأَيْكَةِ لَظَـٰلِمِينَ
15:78 Na hakika watu wa Kichakani walikuwa wenye kudhulumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:79 فَٱنتَقَمْنَا مِنْهُمْ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامٍ مُّبِينٍ
15:79 Kwa hivyo tukawaadhibu. Na nchi mbili hizi ziko kwenye njia ilio wazi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:80 وَلَقَدْ كَذَّبَ أَصْحَـٰبُ ٱلْحِجْرِ ٱلْمُرْسَلِينَ
15:80 Na bila ya shaka wakaazi wa Hijr waliwakanusha Mitume. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:81 وَءَاتَيْنَـٰهُمْ ءَايَـٰتِنَا فَكَانُوا۟ عَنْهَا مُعْرِضِينَ
15:81 Na tuliwapa ishara zetu, nao wakazipuuza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:82 وَكَانُوا۟ يَنْحِتُونَ مِنَ ٱلْجِبَالِ بُيُوتًا ءَامِنِينَ
15:82 Nao walikuwa wakichonga majumba katika milima kwa amani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:83 فَأَخَذَتْهُمُ ٱلصَّيْحَةُ مُصْبِحِينَ
15:83 Basi ukelele ukawatwaa asubuhi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:84 فَمَآ أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ
15:84 Hayakuwafaa waliyo kuwa wakiyachuma. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:85 وَمَا خَلَقْنَا ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَآ إِلَّا بِٱلْحَقِّ ۗ وَإِنَّ ٱلسَّاعَةَ لَـَٔاتِيَةٌ ۖ فَٱصْفَحِ ٱلصَّفْحَ ٱلْجَمِيلَ
15:85 Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ila kwa ajili ya Haki. Na hakika Kiyama kitafika. Basi samehe msamaha mzuri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:86 إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلْخَلَّـٰقُ ٱلْعَلِيمُ
15:86 Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji Mjuzi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:87 وَلَقَدْ ءَاتَيْنَـٰكَ سَبْعًا مِّنَ ٱلْمَثَانِى وَٱلْقُرْءَانَ ٱلْعَظِيمَ
15:87 Na tumekupa Aya saba zinazo somwa mara kwa mara, na Qur'ani Tukufu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:88 لَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِۦٓ أَزْوَٰجًا مِّنْهُمْ وَلَا تَحْزَنْ عَلَيْهِمْ وَٱخْفِضْ جَنَاحَكَ لِلْمُؤْمِنِينَ
15:88 Usivitumbulie macho yako vitu tulivyo waneemesha makundi fulani kati yao, wala usiwahuzunikie. Na wainamishie bawa lako (la huruma) Waumini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:89 وَقُلْ إِنِّىٓ أَنَا ٱلنَّذِيرُ ٱلْمُبِينُ
15:89 Na sema: Hakika mimi ni mwonyaji mwenye kubainisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:90 كَمَآ أَنزَلْنَا عَلَى ٱلْمُقْتَسِمِينَ
15:90 Kama hivyo tuliwateremshia walio gawa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:91 ٱلَّذِينَ جَعَلُوا۟ ٱلْقُرْءَانَ عِضِينَ
15:91 Ambao wakaifanya Qur'ani vipande vipande. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:92 فَوَرَبِّكَ لَنَسْـَٔلَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ
15:92 Basi Naapa kwa Mola wako Mlezi! Tutawahoji wote, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:93 عَمَّا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ
15:93 Kwa waliyo kuwa wakiyatenda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:94 فَٱصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ ٱلْمُشْرِكِينَ
15:94 Basi wewe yatangaze uliyo amrishwa, na jitenge na washirikina. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:95 إِنَّا كَفَيْنَـٰكَ ٱلْمُسْتَهْزِءِينَ
15:95 Hakika Sisi tunatosha kukukinga na wanao kejeli. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:96 ٱلَّذِينَ يَجْعَلُونَ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ
15:96 Hao wanao fanya kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu yupo mungu mwingine. Basi, watakuja jua! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:97 وَلَقَدْ نَعْلَمُ أَنَّكَ يَضِيقُ صَدْرُكَ بِمَا يَقُولُونَ
15:97 Na Sisi tunajua kwa hakika kuwa wewe kifua chako kinaona dhiki kwa hayo wayasemayo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:98 فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَكُن مِّنَ ٱلسَّـٰجِدِينَ
15:98 Basi mtakase Mola wako Mlezi kwa kumhimidi, na uwe miongoni wanao msujudia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

15:99 وَٱعْبُدْ رَبَّكَ حَتَّىٰ يَأْتِيَكَ ٱلْيَقِينُ
15:99 Na muabudu Mola wako Mlezi mpaka ikufikie Yakini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)