Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

26 Ash-Shu`arā' ٱلشُّعَرَاء

< Previous   227 Āyah   The Poets      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

26:1 طسٓمٓ
26:1 T'aa Siin Miim. (T'. S. M.) - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:2 تِلْكَ ءَايَـٰتُ ٱلْكِتَـٰبِ ٱلْمُبِينِ
26:2 Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:3 لَعَلَّكَ بَـٰخِعٌ نَّفْسَكَ أَلَّا يَكُونُوا۟ مُؤْمِنِينَ
26:3 Huenda labda ukajikera nafsi yako kwa kuwa hawawi Waumini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:4 إِن نَّشَأْ نُنَزِّلْ عَلَيْهِم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ ءَايَةً فَظَلَّتْ أَعْنَـٰقُهُمْ لَهَا خَـٰضِعِينَ
26:4 Tunge penda tungeli wateremshia kutoka mbinguni Ishara zikanyenyekea shingo zao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:5 وَمَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّنَ ٱلرَّحْمَـٰنِ مُحْدَثٍ إِلَّا كَانُوا۟ عَنْهُ مُعْرِضِينَ
26:5 Wala hauwafikii ukumbusho mpya kutoka kwa Arrahman ila wao hujitenga nao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:6 فَقَدْ كَذَّبُوا۟ فَسَيَأْتِيهِمْ أَنۢبَـٰٓؤُا۟ مَا كَانُوا۟ بِهِۦ يَسْتَهْزِءُونَ
26:6 Kwa yakini wamekanusha; kwa hivyo zitakuja wafikia khabari za yale waliyo kuwa wakiyafanyia mzaha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:7 أَوَلَمْ يَرَوْا۟ إِلَى ٱلْأَرْضِ كَمْ أَنۢبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ
26:7 Je! Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:8 إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
26:8 Hakika katika haya zipo Ishara. Lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:9 وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
26:9 Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:10 وَإِذْ نَادَىٰ رَبُّكَ مُوسَىٰٓ أَنِ ٱئْتِ ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ
26:10 Na Mola wako Mlezi, alipo mwita Musa, akamwambia: Fika kwa watu madhaalimu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:11 قَوْمَ فِرْعَوْنَ ۚ أَلَا يَتَّقُونَ
26:11 Watu wa Firauni. Hawaogopi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:12 قَالَ رَبِّ إِنِّىٓ أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ
26:12 Akasema: Hakika mimi nachelea wasinikanushe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:13 وَيَضِيقُ صَدْرِى وَلَا يَنطَلِقُ لِسَانِى فَأَرْسِلْ إِلَىٰ هَـٰرُونَ
26:13 Na kifua changu kina dhiki, na ulimi wangu haukunjuki vyema. Basi mtumie ujumbe Harun. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:14 وَلَهُمْ عَلَىَّ ذَنۢبٌ فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ
26:14 Na wao wana kisasi juu yangu, kwa hivyo naogopa wasije kuniuwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:15 قَالَ كَلَّا ۖ فَٱذْهَبَا بِـَٔايَـٰتِنَآ ۖ إِنَّا مَعَكُم مُّسْتَمِعُونَ
26:15 Akasema: Siyo hivyo kabisa! Nendeni na miujiza yetu. Hakika Sisi tu pamoja nanyi, tunasikiliza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:16 فَأْتِيَا فِرْعَوْنَ فَقُولَآ إِنَّا رَسُولُ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
26:16 Basi mfikieni Firauni na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:17 أَنْ أَرْسِلْ مَعَنَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ
26:17 Waachilie Wana wa Israili wende nasi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:18 قَالَ أَلَمْ نُرَبِّكَ فِينَا وَلِيدًا وَلَبِثْتَ فِينَا مِنْ عُمُرِكَ سِنِينَ
26:18 (Firauni) akasema: Sisi hatukukulea wewe utotoni, na ukakaa kwetu katika umri wako miaka mingi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:19 وَفَعَلْتَ فَعْلَتَكَ ٱلَّتِى فَعَلْتَ وَأَنتَ مِنَ ٱلْكَـٰفِرِينَ
26:19 Na ukatenda kitendo chako ulicho tenda, nawe ukawa miongoni mwa wasio na shukrani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:20 قَالَ فَعَلْتُهَآ إِذًا وَأَنَا۠ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ
26:20 (Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwa miongoni mwa wale walio potea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:21 فَفَرَرْتُ مِنكُمْ لَمَّا خِفْتُكُمْ فَوَهَبَ لِى رَبِّى حُكْمًا وَجَعَلَنِى مِنَ ٱلْمُرْسَلِينَ
26:21 Basi nikakukimbieni nilipo kuogopeni, tena Mola wangu Mlezi akanitunukia hukumu, na akanijaalia niwe miongoni mwa Mitume. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:22 وَتِلْكَ نِعْمَةٌ تَمُنُّهَا عَلَىَّ أَنْ عَبَّدتَّ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ
26:22 Na hiyo ndiyo neema ya kunisumbulia, na wewe umewatia utumwani Wana wa Israili? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:23 قَالَ فِرْعَوْنُ وَمَا رَبُّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
26:23 Firauni akasema: Na nani huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:24 قَالَ رَبُّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَآ ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ
26:24 Akasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi ni wenye yakini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:25 قَالَ لِمَنْ حَوْلَهُۥٓ أَلَا تَسْتَمِعُونَ
26:25 (Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:26 قَالَ رَبُّكُمْ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلْأَوَّلِينَ
26:26 (Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba zenu wa kwanza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:27 قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ ٱلَّذِىٓ أُرْسِلَ إِلَيْكُمْ لَمَجْنُونٌ
26:27 (Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenu ni mwendawazimu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:28 قَالَ رَبُّ ٱلْمَشْرِقِ وَٱلْمَغْرِبِ وَمَا بَيْنَهُمَآ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ
26:28 (Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatia akilini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:29 قَالَ لَئِنِ ٱتَّخَذْتَ إِلَـٰهًا غَيْرِى لَأَجْعَلَنَّكَ مِنَ ٱلْمَسْجُونِينَ
26:29 (Firauni) akasema: Ukimfuata mungu mwengine asiye kuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga gerezani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:30 قَالَ أَوَلَوْ جِئْتُكَ بِشَىْءٍ مُّبِينٍ
26:30 Akasema: Je! Ijapo kuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:31 قَالَ فَأْتِ بِهِۦٓ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
26:31 Akasema: Kilete basi, kama wewe ni katika wasemao kweli. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:32 فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ
26:32 Basi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wa kuonekana dhaahiri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:33 وَنَزَعَ يَدَهُۥ فَإِذَا هِىَ بَيْضَآءُ لِلنَّـٰظِرِينَ
26:33 Na akautoa mkono wake, na mara ukawa mweupe kwa watazamao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:34 قَالَ لِلْمَلَإِ حَوْلَهُۥٓ إِنَّ هَـٰذَا لَسَـٰحِرٌ عَلِيمٌ
26:34 (Firauni) akawaambia waheshimiwa walio mzunguka: Hakika huyu ni mchawi mtaalamu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:35 يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُم بِسِحْرِهِۦ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ
26:35 Anataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna shauri gani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:36 قَالُوٓا۟ أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَٱبْعَثْ فِى ٱلْمَدَآئِنِ حَـٰشِرِينَ
26:36 Wakasema: Mpe muda yeye na nduguye na uwatume mijini wapigao mbiu ya mgambo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:37 يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَحَّارٍ عَلِيمٍ
26:37 Wakuletee kila mchawi bingwa mtaalamu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:38 فَجُمِعَ ٱلسَّحَرَةُ لِمِيقَـٰتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ
26:38 Basi wakakusanywa wachawi wakati na siku maalumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:39 وَقِيلَ لِلنَّاسِ هَلْ أَنتُم مُّجْتَمِعُونَ
26:39 Na watu wakaambiwa: Je! Mtakusanyika? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:40 لَعَلَّنَا نَتَّبِعُ ٱلسَّحَرَةَ إِن كَانُوا۟ هُمُ ٱلْغَـٰلِبِينَ
26:40 Huenda tutawafuata wachawi wakiwa wao ndio watakao shinda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:41 فَلَمَّا جَآءَ ٱلسَّحَرَةُ قَالُوا۟ لِفِرْعَوْنَ أَئِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ ٱلْغَـٰلِبِينَ
26:41 Basi walipo kuja wachawi wakamwambia Firauni: Je! Tutapata ujira tukiwa sisi ndio tulio shinda? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:42 قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ إِذًا لَّمِنَ ٱلْمُقَرَّبِينَ
26:42 Naam! Na hakika mtakuwa katika watu wa mbele. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:43 قَالَ لَهُم مُّوسَىٰٓ أَلْقُوا۟ مَآ أَنتُم مُّلْقُونَ
26:43 Musa akwaambia: Tupeni mnavyo taka kutupa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:44 فَأَلْقَوْا۟ حِبَالَهُمْ وَعِصِيَّهُمْ وَقَالُوا۟ بِعِزَّةِ فِرْعَوْنَ إِنَّا لَنَحْنُ ٱلْغَـٰلِبُونَ
26:44 Basi wakatupa kamba zao na fimbo zao, na wakasema: Kwa nguvu za Firauni hakika sisi hapana shaka ni wenye kushinda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:45 فَأَلْقَىٰ مُوسَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِىَ تَلْقَفُ مَا يَأْفِكُونَ
26:45 Musa tena akatupa fimbo yake, nayo mara ikavimeza walivyo vizua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:46 فَأُلْقِىَ ٱلسَّحَرَةُ سَـٰجِدِينَ
26:46 Hapo wachawi walipinduka wakasujudu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:47 قَالُوٓا۟ ءَامَنَّا بِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
26:47 Wakasema: Tunamuamini Mola Mlezi wa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:48 رَبِّ مُوسَىٰ وَهَـٰرُونَ
26:48 Mola Mlezi wa Musa na Harun. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:49 قَالَ ءَامَنتُمْ لَهُۥ قَبْلَ أَنْ ءَاذَنَ لَكُمْ ۖ إِنَّهُۥ لَكَبِيرُكُمُ ٱلَّذِى عَلَّمَكُمُ ٱلسِّحْرَ فَلَسَوْفَ تَعْلَمُونَ ۚ لَأُقَطِّعَنَّ أَيْدِيَكُمْ وَأَرْجُلَكُم مِّنْ خِلَـٰفٍ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ أَجْمَعِينَ
26:49 (Firauni) akasema: Je! Mmemuamini kabla sijakuruhusuni? Bila ya shaka yeye basi ndiye mkubwa wenu aliye kufunzeni uchawi. Basi mtakuja jua! Nitakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutafautisha. Na nitakubandikeni misalabani nyote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:50 قَالُوا۟ لَا ضَيْرَ ۖ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ
26:50 Wakasema: Haidhuru, kwani sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:51 إِنَّا نَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لَنَا رَبُّنَا خَطَـٰيَـٰنَآ أَن كُنَّآ أَوَّلَ ٱلْمُؤْمِنِينَ
26:51 Hakika sisi tunatumai Mola wetu Mlezi atatusamehe makosa yetu, kwa kuwa ndio wa kwanza wa kuamini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:52 ۞ وَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنْ أَسْرِ بِعِبَادِىٓ إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ
26:52 Na tulimuamrisha Musa kwa wahyi: Nenda na waja wangu wakati wa usiku. Kwa hakika mtafuatwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:53 فَأَرْسَلَ فِرْعَوْنُ فِى ٱلْمَدَآئِنِ حَـٰشِرِينَ
26:53 Basi Firauni akawatuma mijini wapiga mbiu za mgambo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:54 إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ لَشِرْذِمَةٌ قَلِيلُونَ
26:54 (Wakieneza): Hakika hawa ni kikundi kidogo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:55 وَإِنَّهُمْ لَنَا لَغَآئِظُونَ
26:55 Nao wanatuudhi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:56 وَإِنَّا لَجَمِيعٌ حَـٰذِرُونَ
26:56 Na sisi ni wengi, wenye kuchukua hadhari. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:57 فَأَخْرَجْنَـٰهُم مِّن جَنَّـٰتٍ وَعُيُونٍ
26:57 Basi tukawatoa katika mabustani na chemchem, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:58 وَكُنُوزٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ
26:58 Na makhazina, na vyeo vya hishima, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:59 كَذَٰلِكَ وَأَوْرَثْنَـٰهَا بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ
26:59 Kadhaalika; na tukawarithisha hayo Wana wa Israili. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:60 فَأَتْبَعُوهُم مُّشْرِقِينَ
26:60 Basi wakawafuata lilipo chomoza jua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:61 فَلَمَّا تَرَٰٓءَا ٱلْجَمْعَانِ قَالَ أَصْحَـٰبُ مُوسَىٰٓ إِنَّا لَمُدْرَكُونَ
26:61 Na yalipo onana majeshi mawili haya, watu wa Musa wakasema: Hakika sisi bila ya shaka tumepatikana! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:62 قَالَ كَلَّآ ۖ إِنَّ مَعِىَ رَبِّى سَيَهْدِينِ
26:62 (Musa) akasema: Hasha! Hakika yu pamoja nami Mola wangu Mlezi. Yeye ataniongoa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:63 فَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنِ ٱضْرِب بِّعَصَاكَ ٱلْبَحْرَ ۖ فَٱنفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍ كَٱلطَّوْدِ ٱلْعَظِيمِ
26:63 Tulimletea wahyi Musa tukamwambia: Piga bahari kwa fimbo yako. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama mlima mkubwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:64 وَأَزْلَفْنَا ثَمَّ ٱلْـَٔاخَرِينَ
26:64 Na tukawajongeza hapo wale wengine. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:65 وَأَنجَيْنَا مُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُۥٓ أَجْمَعِينَ
26:65 Tukawaokoa Musa na walio kuwa pamoja naye wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:66 ثُمَّ أَغْرَقْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ
26:66 Kisha tukawazamisha hao wengine. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:67 إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
26:67 Hakika bila ya shaka katika hayo ipo Ishara; lakini wengi wao si katika wenye kuamini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:68 وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
26:68 Na kwa hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:69 وَٱتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ إِبْرَٰهِيمَ
26:69 Na wasomee khabari za Ibrahim. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:70 إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِۦ مَا تَعْبُدُونَ
26:70 Alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Mnaabudu nini? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:71 قَالُوا۟ نَعْبُدُ أَصْنَامًا فَنَظَلُّ لَهَا عَـٰكِفِينَ
26:71 Wakasema: Tunaabudu masanamu, daima tunayanyenyekea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:72 قَالَ هَلْ يَسْمَعُونَكُمْ إِذْ تَدْعُونَ
26:72 Akasema: Je! Yanakusikieni mnapo yaita? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:73 أَوْ يَنفَعُونَكُمْ أَوْ يَضُرُّونَ
26:73 Au yanakufaeni, au yanakudhuruni? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:74 قَالُوا۟ بَلْ وَجَدْنَآ ءَابَآءَنَا كَذَٰلِكَ يَفْعَلُونَ
26:74 Wakasema: Bali tumewakuta baba zetu wakifanya hivyo hivyo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:75 قَالَ أَفَرَءَيْتُم مَّا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ
26:75 Je! Mmewaona hawa mnao waabudu- - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:76 أَنتُمْ وَءَابَآؤُكُمُ ٱلْأَقْدَمُونَ
26:76 Nyinyi na baba zenu wa zamani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:77 فَإِنَّهُمْ عَدُوٌّ لِّىٓ إِلَّا رَبَّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
26:77 Kwani hakika hao ni adui zangu, isipo kuwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:78 ٱلَّذِى خَلَقَنِى فَهُوَ يَهْدِينِ
26:78 Ambaye ndiye aliye niumba, na Yeye ndiye ananiongoa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:79 وَٱلَّذِى هُوَ يُطْعِمُنِى وَيَسْقِينِ
26:79 Na ambaye ndiye ananilisha na kuninywesha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:80 وَإِذَا مَرِضْتُ فَهُوَ يَشْفِينِ
26:80 Na ninapo ugua ni Yeye ndiye anaye niponesha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:81 وَٱلَّذِى يُمِيتُنِى ثُمَّ يُحْيِينِ
26:81 Na ambaye atanifisha, na kisha atanihuisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:82 وَٱلَّذِىٓ أَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لِى خَطِيٓـَٔتِى يَوْمَ ٱلدِّينِ
26:82 Na ambaye ndiye ninaye mtumai kunisamehe makosa yangu Siku ya Malipo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:83 رَبِّ هَبْ لِى حُكْمًا وَأَلْحِقْنِى بِٱلصَّـٰلِحِينَ
26:83 Mola wangu Mlezi! Nitunukie hukumu na uniunganishe na watendao mema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:84 وَٱجْعَل لِّى لِسَانَ صِدْقٍ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ
26:84 Na unijaalie nitajwe kwa wema na watu watakao kuja baadaye. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:85 وَٱجْعَلْنِى مِن وَرَثَةِ جَنَّةِ ٱلنَّعِيمِ
26:85 Na unijaalie katika warithi wa Bustani za neema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:86 وَٱغْفِرْ لِأَبِىٓ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ
26:86 Na umsamehe baba yangu, kwani hakika alikuwa miongoni mwa wapotovu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:87 وَلَا تُخْزِنِى يَوْمَ يُبْعَثُونَ
26:87 Wala usinihizi Siku watapo fufuliwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:88 يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌ وَلَا بَنُونَ
26:88 Siku ambayo kwamba mali hayato faa kitu wala wana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:89 إِلَّا مَنْ أَتَى ٱللَّهَ بِقَلْبٍ سَلِيمٍ
26:89 Isipo kuwa mwenye kumjia Mwenyezi Mungu na moyo safi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:90 وَأُزْلِفَتِ ٱلْجَنَّةُ لِلْمُتَّقِينَ
26:90 Na Pepo itasogezwa kwa wachamngu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:91 وَبُرِّزَتِ ٱلْجَحِيمُ لِلْغَاوِينَ
26:91 Na Jahannamu itadhihirishwa kwa wapotovu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:92 وَقِيلَ لَهُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَعْبُدُونَ
26:92 Na wataambiwa: Wako wapi mlio kuwa mkiwaabudu - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:93 مِن دُونِ ٱللَّهِ هَلْ يَنصُرُونَكُمْ أَوْ يَنتَصِرُونَ
26:93 Badala ya Mwenyezi Mungu? Je! Wanakusaidieni, au wanajisaidia wenyewe? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:94 فَكُبْكِبُوا۟ فِيهَا هُمْ وَٱلْغَاوُۥنَ
26:94 Basi watavurumizwa humo wao na hao wakosefu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:95 وَجُنُودُ إِبْلِيسَ أَجْمَعُونَ
26:95 Na majeshi ya Ibilisi yote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:96 قَالُوا۟ وَهُمْ فِيهَا يَخْتَصِمُونَ
26:96 Watasema, na hali ya kuwa wanazozana humo: - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:97 تَٱللَّهِ إِن كُنَّا لَفِى ضَلَـٰلٍ مُّبِينٍ
26:97 Wallahi! Kwa yakini tulikuwa katika upotovu ulio dhaahiri, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:98 إِذْ نُسَوِّيكُم بِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
26:98 Tulipo kufanyeni ni sawa na Mola Mlezi wa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:99 وَمَآ أَضَلَّنَآ إِلَّا ٱلْمُجْرِمُونَ
26:99 Na hawakutupoteza ila wale wakosefu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:100 فَمَا لَنَا مِن شَـٰفِعِينَ
26:100 Basi hatuna waombezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:101 وَلَا صَدِيقٍ حَمِيمٍ
26:101 Wala rafiki wa dhati. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:102 فَلَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَكُونَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ
26:102 Laiti tungeli pata kurejea tena tungeli kuwa katika Waumini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:103 إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
26:103 Hakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:104 وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
26:104 Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:105 كَذَّبَتْ قَوْمُ نُوحٍ ٱلْمُرْسَلِينَ
26:105 Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:106 إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ نُوحٌ أَلَا تَتَّقُونَ
26:106 Alipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:107 إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ
26:107 Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:108 فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
26:108 Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:109 وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
26:109 Na sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:110 فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
26:110 Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:111 ۞ قَالُوٓا۟ أَنُؤْمِنُ لَكَ وَٱتَّبَعَكَ ٱلْأَرْذَلُونَ
26:111 Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni watu wa chini? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:112 قَالَ وَمَا عِلْمِى بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ
26:112 Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:113 إِنْ حِسَابُهُمْ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّى ۖ لَوْ تَشْعُرُونَ
26:113 Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli tambua! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:114 وَمَآ أَنَا۠ بِطَارِدِ ٱلْمُؤْمِنِينَ
26:114 Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:115 إِنْ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٌ مُّبِينٌ
26:115 Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri shaahiri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:116 قَالُوا۟ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ يَـٰنُوحُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمَرْجُومِينَ
26:116 Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:117 قَالَ رَبِّ إِنَّ قَوْمِى كَذَّبُونِ
26:117 Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:118 فَٱفْتَحْ بَيْنِى وَبَيْنَهُمْ فَتْحًا وَنَجِّنِى وَمَن مَّعِىَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ
26:118 Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:119 فَأَنجَيْنَـٰهُ وَمَن مَّعَهُۥ فِى ٱلْفُلْكِ ٱلْمَشْحُونِ
26:119 Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika marikebu iliyo sheheni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:120 ثُمَّ أَغْرَقْنَا بَعْدُ ٱلْبَاقِينَ
26:120 Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:121 إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
26:121 Hakika katika haya ipo Ishara, lakini si wengi wao walio kuwa Waumini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:122 وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
26:122 Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:123 كَذَّبَتْ عَادٌ ٱلْمُرْسَلِينَ
26:123 Kina A'd waliwakanusha Mitume. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:124 إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ هُودٌ أَلَا تَتَّقُونَ
26:124 Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamchimngu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:125 إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ
26:125 Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:126 فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
26:126 Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:127 وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
26:127 Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:128 أَتَبْنُونَ بِكُلِّ رِيعٍ ءَايَةً تَعْبَثُونَ
26:128 Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la kufanyia upuuzi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:129 وَتَتَّخِذُونَ مَصَانِعَ لَعَلَّكُمْ تَخْلُدُونَ
26:129 Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi milele! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:130 وَإِذَا بَطَشْتُم بَطَشْتُمْ جَبَّارِينَ
26:130 Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:131 فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
26:131 Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:132 وَٱتَّقُوا۟ ٱلَّذِىٓ أَمَدَّكُم بِمَا تَعْلَمُونَ
26:132 Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:133 أَمَدَّكُم بِأَنْعَـٰمٍ وَبَنِينَ
26:133 Amekupeni wanyama wa kufuga na wana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:134 وَجَنَّـٰتٍ وَعُيُونٍ
26:134 Na mabustani na chemchem. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:135 إِنِّىٓ أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ
26:135 Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:136 قَالُوا۟ سَوَآءٌ عَلَيْنَآ أَوَعَظْتَ أَمْ لَمْ تَكُن مِّنَ ٱلْوَٰعِظِينَ
26:136 Wakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa miongoni mwa watoao mawaidha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:137 إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا خُلُقُ ٱلْأَوَّلِينَ
26:137 Haya si chochote ila ni mtindo wa watu wa tokea zamani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:138 وَمَا نَحْنُ بِمُعَذَّبِينَ
26:138 Wala sisi hatutaadhibiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:139 فَكَذَّبُوهُ فَأَهْلَكْنَـٰهُمْ ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
26:139 Wakamkanusha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila ya shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:140 وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
26:140 Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:141 كَذَّبَتْ ثَمُودُ ٱلْمُرْسَلِينَ
26:141 Kina Thamud waliwakanusha Mitume. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:142 إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ صَـٰلِحٌ أَلَا تَتَّقُونَ
26:142 Alipo waambia ndugu yao Saleh: Je! Hamumchimngu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:143 إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ
26:143 Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:144 فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
26:144 Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:145 وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
26:145 Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:146 أَتُتْرَكُونَ فِى مَا هَـٰهُنَآ ءَامِنِينَ
26:146 Je! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:147 فِى جَنَّـٰتٍ وَعُيُونٍ
26:147 Katika mabustani, na chemchem? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:148 وَزُرُوعٍ وَنَخْلٍ طَلْعُهَا هَضِيمٌ
26:148 Na konde na mitende yenye makole yaliyo wiva. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:149 وَتَنْحِتُونَ مِنَ ٱلْجِبَالِ بُيُوتًا فَـٰرِهِينَ
26:149 Na mnachonga milimani majumba kwa ustadi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:150 فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
26:150 Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:151 وَلَا تُطِيعُوٓا۟ أَمْرَ ٱلْمُسْرِفِينَ
26:151 Wala msit'ii amri za walio pindukia mipaka, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:152 ٱلَّذِينَ يُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ وَلَا يُصْلِحُونَ
26:152 Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:153 قَالُوٓا۟ إِنَّمَآ أَنتَ مِنَ ٱلْمُسَحَّرِينَ
26:153 Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:154 مَآ أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا فَأْتِ بِـَٔايَةٍ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
26:154 Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:155 قَالَ هَـٰذِهِۦ نَاقَةٌ لَّهَا شِرْبٌ وَلَكُمْ شِرْبُ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ
26:155 Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:156 وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابُ يَوْمٍ عَظِيمٍ
26:156 Wala msimguse kwa uwovu, isije ikakushikeni adhabu ya Siku Kubwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:157 فَعَقَرُوهَا فَأَصْبَحُوا۟ نَـٰدِمِينَ
26:157 Lakini wakamuuwa, na wakawa wenye kujuta. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:158 فَأَخَذَهُمُ ٱلْعَذَابُ ۗ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
26:158 Basi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:159 وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
26:159 Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:160 كَذَّبَتْ قَوْمُ لُوطٍ ٱلْمُرْسَلِينَ
26:160 Watu wa Lut'i waliwakanusha Mitume. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:161 إِذْ قَالَ لَهُمْ أَخُوهُمْ لُوطٌ أَلَا تَتَّقُونَ
26:161 Alipo waambia ndugu yao, Lut'i: Je! Hamumchimngu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:162 إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ
26:162 Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu kwenu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:163 فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
26:163 Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:164 وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
26:164 Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:165 أَتَأْتُونَ ٱلذُّكْرَانَ مِنَ ٱلْعَـٰلَمِينَ
26:165 Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:166 وَتَذَرُونَ مَا خَلَقَ لَكُمْ رَبُّكُم مِّنْ أَزْوَٰجِكُم ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ عَادُونَ
26:166 Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:167 قَالُوا۟ لَئِن لَّمْ تَنتَهِ يَـٰلُوطُ لَتَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُخْرَجِينَ
26:167 Wakasema: Ewe Lut'i! Usipo acha, hapana shaka utakuwa miongoni mwa wanao tolewa mji! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:168 قَالَ إِنِّى لِعَمَلِكُم مِّنَ ٱلْقَالِينَ
26:168 Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi kitendo chenu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:169 رَبِّ نَجِّنِى وَأَهْلِى مِمَّا يَعْمَلُونَ
26:169 Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya wayatendayo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:170 فَنَجَّيْنَـٰهُ وَأَهْلَهُۥٓ أَجْمَعِينَ
26:170 Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:171 إِلَّا عَجُوزًا فِى ٱلْغَـٰبِرِينَ
26:171 Isipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:172 ثُمَّ دَمَّرْنَا ٱلْـَٔاخَرِينَ
26:172 Kisha tukawaangamiza wale wengine. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:173 وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَسَآءَ مَطَرُ ٱلْمُنذَرِينَ
26:173 Na tukawanyeshea mvua, basi ni ovu mno mvua ya waliyo onywa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:174 إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
26:174 Hakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:175 وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
26:175 Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:176 كَذَّبَ أَصْحَـٰبُ لْـَٔيْكَةِ ٱلْمُرْسَلِينَ
26:176 Watu wa Machakani waliwakanusha Mitume. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:177 إِذْ قَالَ لَهُمْ شُعَيْبٌ أَلَا تَتَّقُونَ
26:177 Shuaibu alipo waambia: Je! Hamfanyi mkamchamngu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:178 إِنِّى لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ
26:178 Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:179 فَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
26:179 Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:180 وَمَآ أَسْـَٔلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِىَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
26:180 Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:181 ۞ أَوْفُوا۟ ٱلْكَيْلَ وَلَا تَكُونُوا۟ مِنَ ٱلْمُخْسِرِينَ
26:181 Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao punja. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:182 وَزِنُوا۟ بِٱلْقِسْطَاسِ ٱلْمُسْتَقِيمِ
26:182 Na pimeni kwa haki iliyo nyooka; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:183 وَلَا تَبْخَسُوا۟ ٱلنَّاسَ أَشْيَآءَهُمْ وَلَا تَعْثَوْا۟ فِى ٱلْأَرْضِ مُفْسِدِينَ
26:183 Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri kwa ufisadi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:184 وَٱتَّقُوا۟ ٱلَّذِى خَلَقَكُمْ وَٱلْجِبِلَّةَ ٱلْأَوَّلِينَ
26:184 Na mcheni aliye kuumbeni nyinyi na vizazi vilivyo tangulia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:185 قَالُوٓا۟ إِنَّمَآ أَنتَ مِنَ ٱلْمُسَحَّرِينَ
26:185 Wakasema: Hakika wewe ni katika walio rogwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:186 وَمَآ أَنتَ إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُنَا وَإِن نَّظُنُّكَ لَمِنَ ٱلْكَـٰذِبِينَ
26:186 Na wewe si chochote ila ni mtu tu kama sisi, na kwa yakini tunakuona wewe ni katika waongo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:187 فَأَسْقِطْ عَلَيْنَا كِسَفًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّـٰدِقِينَ
26:187 Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:188 قَالَ رَبِّىٓ أَعْلَمُ بِمَا تَعْمَلُونَ
26:188 Akasema: Mola wangu Mlezi anajua zaidi mnayo yatenda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:189 فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمْ عَذَابُ يَوْمِ ٱلظُّلَّةِ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ
26:189 Basi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya siku ya kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:190 إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
26:190 Hakika katika hayo ipo Ishara, lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:191 وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
26:191 Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:192 وَإِنَّهُۥ لَتَنزِيلُ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
26:192 Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:193 نَزَلَ بِهِ ٱلرُّوحُ ٱلْأَمِينُ
26:193 Ameuteremsha Roho muaminifu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:194 عَلَىٰ قَلْبِكَ لِتَكُونَ مِنَ ٱلْمُنذِرِينَ
26:194 Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:195 بِلِسَانٍ عَرَبِىٍّ مُّبِينٍ
26:195 Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:196 وَإِنَّهُۥ لَفِى زُبُرِ ٱلْأَوَّلِينَ
26:196 Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:197 أَوَلَمْ يَكُن لَّهُمْ ءَايَةً أَن يَعْلَمَهُۥ عُلَمَـٰٓؤُا۟ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ
26:197 Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:198 وَلَوْ نَزَّلْنَـٰهُ عَلَىٰ بَعْضِ ٱلْأَعْجَمِينَ
26:198 Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:199 فَقَرَأَهُۥ عَلَيْهِم مَّا كَانُوا۟ بِهِۦ مُؤْمِنِينَ
26:199 Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:200 كَذَٰلِكَ سَلَكْنَـٰهُ فِى قُلُوبِ ٱلْمُجْرِمِينَ
26:200 Namna hivi tunaingiza katika nyoyo za wakosefu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:201 لَا يُؤْمِنُونَ بِهِۦ حَتَّىٰ يَرَوُا۟ ٱلْعَذَابَ ٱلْأَلِيمَ
26:201 Hawataiamini mpaka waione adhabu chungu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:202 فَيَأْتِيَهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ
26:202 Basi itawafikia kwa ghafla, na hali hawana khabari. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:203 فَيَقُولُوا۟ هَلْ نَحْنُ مُنظَرُونَ
26:203 Na watasema: Je, tutapewa muhula? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:204 أَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ
26:204 Basi, je, wanaihimiza adhabu yetu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:205 أَفَرَءَيْتَ إِن مَّتَّعْنَـٰهُمْ سِنِينَ
26:205 Waonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:206 ثُمَّ جَآءَهُم مَّا كَانُوا۟ يُوعَدُونَ
26:206 Kisha yakawafikia waliyo kuwa wakiahidiwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:207 مَآ أَغْنَىٰ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يُمَتَّعُونَ
26:207 Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:208 وَمَآ أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ إِلَّا لَهَا مُنذِرُونَ
26:208 Wala hatukuangamiza mji wo wote ila ulikuwa na waonyaji - - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:209 ذِكْرَىٰ وَمَا كُنَّا ظَـٰلِمِينَ
26:209 Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:210 وَمَا تَنَزَّلَتْ بِهِ ٱلشَّيَـٰطِينُ
26:210 Wala Mashet'ani hawakuteremka nayo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:211 وَمَا يَنۢبَغِى لَهُمْ وَمَا يَسْتَطِيعُونَ
26:211 Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:212 إِنَّهُمْ عَنِ ٱلسَّمْعِ لَمَعْزُولُونَ
26:212 Hakika hao wametengwa na kusikia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:213 فَلَا تَدْعُ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ فَتَكُونَ مِنَ ٱلْمُعَذَّبِينَ
26:213 Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:214 وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ ٱلْأَقْرَبِينَ
26:214 Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:215 وَٱخْفِضْ جَنَاحَكَ لِمَنِ ٱتَّبَعَكَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ
26:215 Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa Waumini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:216 فَإِنْ عَصَوْكَ فَقُلْ إِنِّى بَرِىٓءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ
26:216 Na ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitenga mbali na hayo mnayo yatenda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:217 وَتَوَكَّلْ عَلَى ٱلْعَزِيزِ ٱلرَّحِيمِ
26:217 Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:218 ٱلَّذِى يَرَىٰكَ حِينَ تَقُومُ
26:218 Ambaye anakuona unapo simama, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:219 وَتَقَلُّبَكَ فِى ٱلسَّـٰجِدِينَ
26:219 Na mageuko yako kati ya wanao sujudu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:220 إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ
26:220 Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:221 هَلْ أُنَبِّئُكُمْ عَلَىٰ مَن تَنَزَّلُ ٱلشَّيَـٰطِينُ
26:221 Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:222 تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ
26:222 Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:223 يُلْقُونَ ٱلسَّمْعَ وَأَكْثَرُهُمْ كَـٰذِبُونَ
26:223 Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni waongo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:224 وَٱلشُّعَرَآءُ يَتَّبِعُهُمُ ٱلْغَاوُۥنَ
26:224 Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:225 أَلَمْ تَرَ أَنَّهُمْ فِى كُلِّ وَادٍ يَهِيمُونَ
26:225 Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila bonde? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:226 وَأَنَّهُمْ يَقُولُونَ مَا لَا يَفْعَلُونَ
26:226 Na kwamba wao husema wasiyo yatenda? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

26:227 إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ وَذَكَرُوا۟ ٱللَّهَ كَثِيرًا وَٱنتَصَرُوا۟ مِنۢ بَعْدِ مَا ظُلِمُوا۟ ۗ وَسَيَعْلَمُ ٱلَّذِينَ ظَلَمُوٓا۟ أَىَّ مُنقَلَبٍ يَنقَلِبُونَ
26:227 Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)