Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

85 Al-Burūj ٱلْبُرُوج

< Previous   22 Āyah   The Mansions of the Stars      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

85:1 وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلْبُرُوجِ
85:1 Naapa kwa mbingu yenye Buruji! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:2 وَٱلْيَوْمِ ٱلْمَوْعُودِ
85:2 Na kwa siku iliyo ahidiwa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:3 وَشَاهِدٍ وَمَشْهُودٍ
85:3 Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:4 قُتِلَ أَصْحَـٰبُ ٱلْأُخْدُودِ
85:4 Wameangamizwa watu wa makhandaki - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:5 ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلْوَقُودِ
85:5 Yenye moto wenye kuni nyingi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:6 إِذْ هُمْ عَلَيْهَا قُعُودٌ
85:6 Walipo kuwa wamekaa hapo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:7 وَهُمْ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ بِٱلْمُؤْمِنِينَ شُهُودٌ
85:7 Na wao ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:8 وَمَا نَقَمُوا۟ مِنْهُمْ إِلَّآ أَن يُؤْمِنُوا۟ بِٱللَّهِ ٱلْعَزِيزِ ٱلْحَمِيدِ
85:8 Nao hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:9 ٱلَّذِى لَهُۥ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ شَهِيدٌ
85:9 Ambaye anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:10 إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُوا۟ ٱلْمُؤْمِنِينَ وَٱلْمُؤْمِنَـٰتِ ثُمَّ لَمْ يَتُوبُوا۟ فَلَهُمْ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمْ عَذَابُ ٱلْحَرِيقِ
85:10 Hakika walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:11 إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَهُمْ جَنَّـٰتٌ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ ۚ ذَٰلِكَ ٱلْفَوْزُ ٱلْكَبِيرُ
85:11 Hakika walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:12 إِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ
85:12 Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:13 إِنَّهُۥ هُوَ يُبْدِئُ وَيُعِيدُ
85:13 Yeye ndiye anaye anzisha na ndiye anaye rejeza tena, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:14 وَهُوَ ٱلْغَفُورُ ٱلْوَدُودُ
85:14 Naye ni Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:15 ذُو ٱلْعَرْشِ ٱلْمَجِيدُ
85:15 Mwenye Kiti cha Enzi, Mtukufu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:16 فَعَّالٌ لِّمَا يُرِيدُ
85:16 Atendaye ayatakayo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:17 هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلْجُنُودِ
85:17 Je! Zimekuwasilia khabari za majeshi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:18 فِرْعَوْنَ وَثَمُودَ
85:18 Ya Firauni na Thamudi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:19 بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فِى تَكْذِيبٍ
85:19 Lakini walio kufuru wamo katika kukadhibisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:20 وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطٌۢ
85:20 Na Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:21 بَلْ هُوَ قُرْءَانٌ مَّجِيدٌ
85:21 Bali hii ni Qur'ani tukufu - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

85:22 فِى لَوْحٍ مَّحْفُوظٍۭ
85:22 Katika Ubao Ulio Hifadhiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)