Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

87 Al-'A`lá ٱلْأَعْلَىٰ

< Previous   19 Āyah   The Most High      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

87:1 سَبِّحِ ٱسْمَ رَبِّكَ ٱلْأَعْلَى
87:1 Litakase jina la Mola wako Mlezi aliye juu kabisa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:2 ٱلَّذِى خَلَقَ فَسَوَّىٰ
87:2 Aliye umba, na akaweka sawa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:3 وَٱلَّذِى قَدَّرَ فَهَدَىٰ
87:3 Na ambaye amekadiria na akaongoa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:4 وَٱلَّذِىٓ أَخْرَجَ ٱلْمَرْعَىٰ
87:4 Na aliye otesha malisho, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:5 فَجَعَلَهُۥ غُثَآءً أَحْوَىٰ
87:5 Kisha akayafanya makavu, meusi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:6 سَنُقْرِئُكَ فَلَا تَنسَىٰٓ
87:6 Tutakusomesha wala hutasahau, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:7 إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُ ۚ إِنَّهُۥ يَعْلَمُ ٱلْجَهْرَ وَمَا يَخْفَىٰ
87:7 Ila akipenda Mwenyezi Mungu. Hakika Yeye anayajua yaliyo dhaahiri na yaliyo fichikana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:8 وَنُيَسِّرُكَ لِلْيُسْرَىٰ
87:8 Na tutakusahilishia yawe mepesi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:9 فَذَكِّرْ إِن نَّفَعَتِ ٱلذِّكْرَىٰ
87:9 Basi kumbusha, kama kukumbusha kunafaa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:10 سَيَذَّكَّرُ مَن يَخْشَىٰ
87:10 Atakumbuka mwenye kuogopa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:11 وَيَتَجَنَّبُهَا ٱلْأَشْقَى
87:11 Na atajitenga mbali nayo mpotovu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:12 ٱلَّذِى يَصْلَى ٱلنَّارَ ٱلْكُبْرَىٰ
87:12 Ambaye atauingia Moto mkubwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:13 ثُمَّ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحْيَىٰ
87:13 Tena humo hatakufa wala hawi hai. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:14 قَدْ أَفْلَحَ مَن تَزَكَّىٰ
87:14 Hakika amekwisha fanikiwa aliye jitakasa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:15 وَذَكَرَ ٱسْمَ رَبِّهِۦ فَصَلَّىٰ
87:15 Na akakumbuka jina la Mola wake Mlezi, na akasali. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:16 بَلْ تُؤْثِرُونَ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا
87:16 Lakini nyinyi mnakhiari maisha ya dunia! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:17 وَٱلْـَٔاخِرَةُ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰٓ
87:17 Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:18 إِنَّ هَـٰذَا لَفِى ٱلصُّحُفِ ٱلْأُولَىٰ
87:18 Hakika haya yamo katika Vitabu vya mwanzo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

87:19 صُحُفِ إِبْرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ
87:19 Vitabu vya Ibrahimu na Musa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)