Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

92 Al-Layl ٱللَّيْل

< Previous   21 Āyah   The Night      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

92:1 وَٱلَّيْلِ إِذَا يَغْشَىٰ
92:1 Naapa kwa usiku unapo funika! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:2 وَٱلنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ
92:2 Na mchana unapo dhihiri! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:3 وَمَا خَلَقَ ٱلذَّكَرَ وَٱلْأُنثَىٰٓ
92:3 Na kwa Aliye umba dume na jike! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:4 إِنَّ سَعْيَكُمْ لَشَتَّىٰ
92:4 Hakika juhudi zenu bila ya shaka ni mbali mbali. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:5 فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَٱتَّقَىٰ
92:5 Ama mwenye kutoa na akamchamngu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:6 وَصَدَّقَ بِٱلْحُسْنَىٰ
92:6 Na akaliwafiki lilio jema, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:7 فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلْيُسْرَىٰ
92:7 Tutamsahilishia yawe mepesi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:8 وَأَمَّا مَنۢ بَخِلَ وَٱسْتَغْنَىٰ
92:8 Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:9 وَكَذَّبَ بِٱلْحُسْنَىٰ
92:9 Na akakanusha lilio jema, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:10 فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلْعُسْرَىٰ
92:10 Tutamsahilishia yawe mazito! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:11 وَمَا يُغْنِى عَنْهُ مَالُهُۥٓ إِذَا تَرَدَّىٰٓ
92:11 Na mali yake yatamfaa nini atapo kuwa anadidimia? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:12 إِنَّ عَلَيْنَا لَلْهُدَىٰ
92:12 Hakika ni juu yetu kuonyesha uwongofu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:13 وَإِنَّ لَنَا لَلْـَٔاخِرَةَ وَٱلْأُولَىٰ
92:13 Na hakika ni yetu Sisi Akhera na dunia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:14 فَأَنذَرْتُكُمْ نَارًا تَلَظَّىٰ
92:14 Basi nakuonyeni na Moto unao waka! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:15 لَا يَصْلَىٰهَآ إِلَّا ٱلْأَشْقَى
92:15 Hatauingia ila mwovu kabisa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:16 ٱلَّذِى كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
92:16 Anaye kadhibisha na kupa mgongo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:17 وَسَيُجَنَّبُهَا ٱلْأَتْقَى
92:17 Na mchamngu ataepushwa nao, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:18 ٱلَّذِى يُؤْتِى مَالَهُۥ يَتَزَكَّىٰ
92:18 Ambaye hutoa mali yake kwa ajili ya kujitakasa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:19 وَمَا لِأَحَدٍ عِندَهُۥ مِن نِّعْمَةٍ تُجْزَىٰٓ
92:19 Na wala si kwa kuwa yupo yeyote aliye mfanyia hisani ndio anamlipa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:20 إِلَّا ٱبْتِغَآءَ وَجْهِ رَبِّهِ ٱلْأَعْلَىٰ
92:20 Ila ni kutaka radhi ya Mola wake Mlezi aliye juu kabisa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

92:21 وَلَسَوْفَ يَرْضَىٰ
92:21 Naye atakuja ridhika! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)