Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

83 Al-Muţaffifīn ٱلْمُطَفِّفِين

< Previous   36 Āyah   The Defrauding      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

83:1 وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ
83:1 Ole wao hao wapunjao! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:2 ٱلَّذِينَ إِذَا ٱكْتَالُوا۟ عَلَى ٱلنَّاسِ يَسْتَوْفُونَ
83:2 Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:3 وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ
83:3 Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:4 أَلَا يَظُنُّ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ
83:4 Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:5 لِيَوْمٍ عَظِيمٍ
83:5 Katika Siku iliyo kuu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:6 يَوْمَ يَقُومُ ٱلنَّاسُ لِرَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
83:6 Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:7 كَلَّآ إِنَّ كِتَـٰبَ ٱلْفُجَّارِ لَفِى سِجِّينٍ
83:7 Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:8 وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا سِجِّينٌ
83:8 Unajua nini Sijjin? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:9 كِتَـٰبٌ مَّرْقُومٌ
83:9 Kitabu kilicho andikwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:10 وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
83:10 Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:11 ٱلَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ ٱلدِّينِ
83:11 Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:12 وَمَا يُكَذِّبُ بِهِۦٓ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ
83:12 Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:13 إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ءَايَـٰتُنَا قَالَ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ
83:13 Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:14 كَلَّا ۖ بَلْ ۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا۟ يَكْسِبُونَ
83:14 Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:15 كَلَّآ إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ
83:15 Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:16 ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُوا۟ ٱلْجَحِيمِ
83:16 Kisha wataingia Motoni! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:17 ثُمَّ يُقَالُ هَـٰذَا ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
83:17 Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:18 كَلَّآ إِنَّ كِتَـٰبَ ٱلْأَبْرَارِ لَفِى عِلِّيِّينَ
83:18 Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:19 وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا عِلِّيُّونَ
83:19 Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:20 كِتَـٰبٌ مَّرْقُومٌ
83:20 Kitabu kilicho andikwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:21 يَشْهَدُهُ ٱلْمُقَرَّبُونَ
83:21 Wanakishuhudia walio karibishwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:22 إِنَّ ٱلْأَبْرَارَ لَفِى نَعِيمٍ
83:22 Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:23 عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
83:23 Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:24 تَعْرِفُ فِى وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ ٱلنَّعِيمِ
83:24 Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:25 يُسْقَوْنَ مِن رَّحِيقٍ مَّخْتُومٍ
83:25 Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:26 خِتَـٰمُهُۥ مِسْكٌ ۚ وَفِى ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ ٱلْمُتَنَـٰفِسُونَ
83:26 Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:27 وَمِزَاجُهُۥ مِن تَسْنِيمٍ
83:27 Na mchanganyiko wake ni Tasniim, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:28 عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا ٱلْمُقَرَّبُونَ
83:28 Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:29 إِنَّ ٱلَّذِينَ أَجْرَمُوا۟ كَانُوا۟ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ يَضْحَكُونَ
83:29 Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:30 وَإِذَا مَرُّوا۟ بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ
83:30 Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:31 وَإِذَا ٱنقَلَبُوٓا۟ إِلَىٰٓ أَهْلِهِمُ ٱنقَلَبُوا۟ فَكِهِينَ
83:31 Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:32 وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوٓا۟ إِنَّ هَـٰٓؤُلَآءِ لَضَآلُّونَ
83:32 Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:33 وَمَآ أُرْسِلُوا۟ عَلَيْهِمْ حَـٰفِظِينَ
83:33 Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:34 فَٱلْيَوْمَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ مِنَ ٱلْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ
83:34 Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:35 عَلَى ٱلْأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
83:35 Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

83:36 هَلْ ثُوِّبَ ٱلْكُفَّارُ مَا كَانُوا۟ يَفْعَلُونَ
83:36 Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)