Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

84 Al-'Inshiqāq ٱلْإِنْشِقَاق

< Previous   25 Āyah   The Sundering      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

84:1 إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنشَقَّتْ
84:1 Itapo chanika mbingu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:2 وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ
84:2 Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:3 وَإِذَا ٱلْأَرْضُ مُدَّتْ
84:3 Na ardhi itakapo tanuliwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:4 وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ
84:4 Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:5 وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ
84:5 Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:6 يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْإِنسَـٰنُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدْحًا فَمُلَـٰقِيهِ
84:6 Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:7 فَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ
84:7 Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:8 فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا
84:8 Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:9 وَيَنقَلِبُ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ مَسْرُورًا
84:9 Na arudi kwa ahali zake na furaha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:10 وَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ وَرَآءَ ظَهْرِهِۦ
84:10 Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:11 فَسَوْفَ يَدْعُوا۟ ثُبُورًا
84:11 Basi huyo ataomba kuteketea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:12 وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا
84:12 Na ataingia Motoni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:13 إِنَّهُۥ كَانَ فِىٓ أَهْلِهِۦ مَسْرُورًا
84:13 Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:14 إِنَّهُۥ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ
84:14 Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:15 بَلَىٰٓ إِنَّ رَبَّهُۥ كَانَ بِهِۦ بَصِيرًا
84:15 Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:16 فَلَآ أُقْسِمُ بِٱلشَّفَقِ
84:16 Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:17 وَٱلَّيْلِ وَمَا وَسَقَ
84:17 Na kwa usiku na unavyo vikusanya, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:18 وَٱلْقَمَرِ إِذَا ٱتَّسَقَ
84:18 Na kwa mwezi unapo pevuka, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:19 لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ
84:19 Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:20 فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ
84:20 Basi wana nini hawaamini? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:21 وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ ٱلْقُرْءَانُ لَا يَسْجُدُونَ ۩
84:21 Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:22 بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ يُكَذِّبُونَ
84:22 Bali walio kufuru wanakanusha tu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:23 وَٱللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ
84:23 Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:24 فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
84:24 Basi wabashirie adhabu chungu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

84:25 إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍۭ
84:25 Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)