Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

86 Aţ-Ţāriq ٱلطَّارِق

< Previous   17 Āyah   The Nightcommer      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

86:1 وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ
86:1 Naapa kwa mbingu na Kinacho kuja usiku! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:2 وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ
86:2 Na nini kitakacho kujuulisha ni nini hicho Kinacho kuja usiku? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:3 ٱلنَّجْمُ ٱلثَّاقِبُ
86:3 Ni Nyota yenye mwanga mkali. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:4 إِن كُلُّ نَفْسٍ لَّمَّا عَلَيْهَا حَافِظٌ
86:4 Hapana nafsi ila inayo mwangalizi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:5 فَلْيَنظُرِ ٱلْإِنسَـٰنُ مِمَّ خُلِقَ
86:5 Hebu naajitazame mwanaadamu ameumbwa kwa kitu gani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:6 خُلِقَ مِن مَّآءٍ دَافِقٍ
86:6 Ameumbwa kwa maji yatokayo kwa kuchupa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:7 يَخْرُجُ مِنۢ بَيْنِ ٱلصُّلْبِ وَٱلتَّرَآئِبِ
86:7 Yatokayo baina ya mifupa ya mgongo na mbavu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:8 إِنَّهُۥ عَلَىٰ رَجْعِهِۦ لَقَادِرٌ
86:8 Hakika Yeye ana uweza wa kumrudisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:9 يَوْمَ تُبْلَى ٱلسَّرَآئِرُ
86:9 Siku zitakapo dhihirishwa siri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:10 فَمَا لَهُۥ مِن قُوَّةٍ وَلَا نَاصِرٍ
86:10 Basi hatakuwa na nguvu wala msaidizi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:11 وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلرَّجْعِ
86:11 Naapa kwa mbingu yenye marejeo! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:12 وَٱلْأَرْضِ ذَاتِ ٱلصَّدْعِ
86:12 Na kwa ardhi inayo pasuka! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:13 إِنَّهُۥ لَقَوْلٌ فَصْلٌ
86:13 Hakika hii ni kauli ya kupambanua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:14 وَمَا هُوَ بِٱلْهَزْلِ
86:14 Wala si mzaha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:15 إِنَّهُمْ يَكِيدُونَ كَيْدًا
86:15 Hakika wao wanapanga mpango. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:16 وَأَكِيدُ كَيْدًا
86:16 Na Mimi napanga mpango. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

86:17 فَمَهِّلِ ٱلْكَـٰفِرِينَ أَمْهِلْهُمْ رُوَيْدًۢا
86:17 Basi wape muhula makafiri - wape muhula pole pole. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)