Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

54 Al-Qamar ٱلْقَمَر

< Previous   55 Āyah   The Moon      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

54:1 ٱقْتَرَبَتِ ٱلسَّاعَةُ وَٱنشَقَّ ٱلْقَمَرُ
54:1 Saa imekaribia, na mwezi umepasuka! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:2 وَإِن يَرَوْا۟ ءَايَةً يُعْرِضُوا۟ وَيَقُولُوا۟ سِحْرٌ مُّسْتَمِرٌّ
54:2 Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:3 وَكَذَّبُوا۟ وَٱتَّبَعُوٓا۟ أَهْوَآءَهُمْ ۚ وَكُلُّ أَمْرٍ مُّسْتَقِرٌّ
54:3 Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:4 وَلَقَدْ جَآءَهُم مِّنَ ٱلْأَنۢبَآءِ مَا فِيهِ مُزْدَجَرٌ
54:4 Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:5 حِكْمَةٌۢ بَـٰلِغَةٌ ۖ فَمَا تُغْنِ ٱلنُّذُرُ
54:5 Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:6 فَتَوَلَّ عَنْهُمْ ۘ يَوْمَ يَدْعُ ٱلدَّاعِ إِلَىٰ شَىْءٍ نُّكُرٍ
54:6 Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo linalo chusha; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:7 خُشَّعًا أَبْصَـٰرُهُمْ يَخْرُجُونَ مِنَ ٱلْأَجْدَاثِ كَأَنَّهُمْ جَرَادٌ مُّنتَشِرٌ
54:7 Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige walio tawanyika, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:8 مُّهْطِعِينَ إِلَى ٱلدَّاعِ ۖ يَقُولُ ٱلْكَـٰفِرُونَ هَـٰذَا يَوْمٌ عَسِرٌ
54:8 Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:9 ۞ كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ فَكَذَّبُوا۟ عَبْدَنَا وَقَالُوا۟ مَجْنُونٌ وَٱزْدُجِرَ
54:9 Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:10 فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنِّى مَغْلُوبٌ فَٱنتَصِرْ
54:10 Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:11 فَفَتَحْنَآ أَبْوَٰبَ ٱلسَّمَآءِ بِمَآءٍ مُّنْهَمِرٍ
54:11 Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo miminika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:12 وَفَجَّرْنَا ٱلْأَرْضَ عُيُونًا فَٱلْتَقَى ٱلْمَآءُ عَلَىٰٓ أَمْرٍ قَدْ قُدِرَ
54:12 Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo lilio kadiriwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:13 وَحَمَلْنَـٰهُ عَلَىٰ ذَاتِ أَلْوَٰحٍ وَدُسُرٍ
54:13 Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:14 تَجْرِى بِأَعْيُنِنَا جَزَآءً لِّمَن كَانَ كُفِرَ
54:14 Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:15 وَلَقَد تَّرَكْنَـٰهَآ ءَايَةً فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ
54:15 Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anaye kumbuka? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:16 فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِى وَنُذُرِ
54:16 Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:17 وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ
54:17 Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:18 كَذَّبَتْ عَادٌ فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِى وَنُذُرِ
54:18 Kina A'di walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:19 إِنَّآ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِى يَوْمِ نَحْسٍ مُّسْتَمِرٍّ
54:19 Hakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku korofi mfululizo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:20 تَنزِعُ ٱلنَّاسَ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ مُّنقَعِرٍ
54:20 Ukiwang'oa watu kama vigogo vya mitende vilio ng'olewa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:21 فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِى وَنُذُرِ
54:21 Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:22 وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ
54:22 Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani nyepesi kufahamika; lakini yupo anaye kumbuka? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:23 كَذَّبَتْ ثَمُودُ بِٱلنُّذُرِ
54:23 Thamudi waliwakanusha Waonyaji. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:24 فَقَالُوٓا۟ أَبَشَرًا مِّنَّا وَٰحِدًا نَّتَّبِعُهُۥٓ إِنَّآ إِذًا لَّفِى ضَلَـٰلٍ وَسُعُرٍ
54:24 Wakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:25 أَءُلْقِىَ ٱلذِّكْرُ عَلَيْهِ مِنۢ بَيْنِنَا بَلْ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٌ
54:25 Ni yeye tu aliye teremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mwenye kiburi! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:26 سَيَعْلَمُونَ غَدًا مَّنِ ٱلْكَذَّابُ ٱلْأَشِرُ
54:26 Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:27 إِنَّا مُرْسِلُوا۟ ٱلنَّاقَةِ فِتْنَةً لَّهُمْ فَٱرْتَقِبْهُمْ وَٱصْطَبِرْ
54:27 Hakika Sisi tutawapelekea ngamia jike ili kuwajaribu, basi watazame tu na ustahamili. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:28 وَنَبِّئْهُمْ أَنَّ ٱلْمَآءَ قِسْمَةٌۢ بَيْنَهُمْ ۖ كُلُّ شِرْبٍ مُّحْتَضَرٌ
54:28 Na waambie kwamba maji yatagawanywa baina yao; kila sehemu ya maji itahudhuriwa na aliye khusika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:29 فَنَادَوْا۟ صَاحِبَهُمْ فَتَعَاطَىٰ فَعَقَرَ
54:29 Basi wakamwita mtu wao akaja akamchinja. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:30 فَكَيْفَ كَانَ عَذَابِى وَنُذُرِ
54:30 Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:31 إِنَّآ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ صَيْحَةً وَٰحِدَةً فَكَانُوا۟ كَهَشِيمِ ٱلْمُحْتَظِرِ
54:31 Hakika Sisi tuliwapelekea ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa ya kujengea uwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:32 وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ
54:32 Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:33 كَذَّبَتْ قَوْمُ لُوطٍۭ بِٱلنُّذُرِ
54:33 Kaumu Lut'i nao waliwakadhibisha Waonyaji. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:34 إِنَّآ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ حَاصِبًا إِلَّآ ءَالَ لُوطٍ ۖ نَّجَّيْنَـٰهُم بِسَحَرٍ
54:34 Hakika Sisi tukawapelekea kimbunga cha vijiwe, isipo kuwa wafuasi wa Lut'i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:35 نِّعْمَةً مِّنْ عِندِنَا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِى مَن شَكَرَ
54:35 Kwa neema inayo toka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anaye shukuru. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:36 وَلَقَدْ أَنذَرَهُم بَطْشَتَنَا فَتَمَارَوْا۟ بِٱلنُّذُرِ
54:36 Na hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia shaka hayo maonyo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:37 وَلَقَدْ رَٰوَدُوهُ عَن ضَيْفِهِۦ فَطَمَسْنَآ أَعْيُنَهُمْ فَذُوقُوا۟ عَذَابِى وَنُذُرِ
54:37 Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na tukawaambia: Onjeni basi adhabu na maonyo yangu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:38 وَلَقَدْ صَبَّحَهُم بُكْرَةً عَذَابٌ مُّسْتَقِرٌّ
54:38 Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:39 فَذُوقُوا۟ عَذَابِى وَنُذُرِ
54:39 Basi onjeni adhabu na maonyo yangu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:40 وَلَقَدْ يَسَّرْنَا ٱلْقُرْءَانَ لِلذِّكْرِ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ
54:40 Na hakika tumeisahilisha Qur'ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye kumbuka? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:41 وَلَقَدْ جَآءَ ءَالَ فِرْعَوْنَ ٱلنُّذُرُ
54:41 Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:42 كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا كُلِّهَا فَأَخَذْنَـٰهُمْ أَخْذَ عَزِيزٍ مُّقْتَدِرٍ
54:42 Walizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika kama anavyo shika Mwenye nguvu Mwenye uweza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:43 أَكُفَّارُكُمْ خَيْرٌ مِّنْ أُو۟لَـٰٓئِكُمْ أَمْ لَكُم بَرَآءَةٌ فِى ٱلزُّبُرِ
54:43 Je! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:44 أَمْ يَقُولُونَ نَحْنُ جَمِيعٌ مُّنتَصِرٌ
54:44 Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:45 سَيُهْزَمُ ٱلْجَمْعُ وَيُوَلُّونَ ٱلدُّبُرَ
54:45 Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:46 بَلِ ٱلسَّاعَةُ مَوْعِدُهُمْ وَٱلسَّاعَةُ أَدْهَىٰ وَأَمَرُّ
54:46 Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu zaidi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:47 إِنَّ ٱلْمُجْرِمِينَ فِى ضَلَـٰلٍ وَسُعُرٍ
54:47 Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:48 يَوْمَ يُسْحَبُونَ فِى ٱلنَّارِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ ذُوقُوا۟ مَسَّ سَقَرَ
54:48 Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:49 إِنَّا كُلَّ شَىْءٍ خَلَقْنَـٰهُ بِقَدَرٍ
54:49 Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:50 وَمَآ أَمْرُنَآ إِلَّا وَٰحِدَةٌ كَلَمْحٍۭ بِٱلْبَصَرِ
54:50 Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:51 وَلَقَدْ أَهْلَكْنَآ أَشْيَاعَكُمْ فَهَلْ مِن مُّدَّكِرٍ
54:51 Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye kumbuka? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:52 وَكُلُّ شَىْءٍ فَعَلُوهُ فِى ٱلزُّبُرِ
54:52 Na kila jambo walilo lifanya limo vitabuni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:53 وَكُلُّ صَغِيرٍ وَكَبِيرٍ مُّسْتَطَرٌ
54:53 Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:54 إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّـٰتٍ وَنَهَرٍ
54:54 Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

54:55 فِى مَقْعَدِ صِدْقٍ عِندَ مَلِيكٍ مُّقْتَدِرٍۭ
54:55 Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)