Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

51 Adh-Dhāriyāt ٱلذَّارِيَات

< Previous   60 Āyah   The Winnowing Winds      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

51:1 وَٱلذَّٰرِيَـٰتِ ذَرْوًا
51:1 Naapa kwa pepo zinazo tawanya, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:2 فَٱلْحَـٰمِلَـٰتِ وِقْرًا
51:2 Na zinazo beba mizigo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:3 فَٱلْجَـٰرِيَـٰتِ يُسْرًا
51:3 Na zinazo kwenda kwa wepesi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:4 فَٱلْمُقَسِّمَـٰتِ أَمْرًا
51:4 Na zinazo gawanya kwa amri, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:5 إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٌ
51:5 Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:6 وَإِنَّ ٱلدِّينَ لَوَٰقِعٌ
51:6 Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:7 وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلْحُبُكِ
51:7 Naapa kwa mbingu zenye njia, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:8 إِنَّكُمْ لَفِى قَوْلٍ مُّخْتَلِفٍ
51:8 Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo khitalifiana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:9 يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ
51:9 Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:10 قُتِلَ ٱلْخَرَّٰصُونَ
51:10 Wazushi wameangamizwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:11 ٱلَّذِينَ هُمْ فِى غَمْرَةٍ سَاهُونَ
51:11 Ambao wameghafilika katika ujinga. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:12 يَسْـَٔلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ ٱلدِّينِ
51:12 Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:13 يَوْمَ هُمْ عَلَى ٱلنَّارِ يُفْتَنُونَ
51:13 Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:14 ذُوقُوا۟ فِتْنَتَكُمْ هَـٰذَا ٱلَّذِى كُنتُم بِهِۦ تَسْتَعْجِلُونَ
51:14 Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:15 إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّـٰتٍ وَعُيُونٍ
51:15 Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:16 ءَاخِذِينَ مَآ ءَاتَىٰهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ
51:16 Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya wakifanya mema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:17 كَانُوا۟ قَلِيلًا مِّنَ ٱلَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ
51:17 Walikuwa wakilala kidogo tu usiku. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:18 وَبِٱلْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ
51:18 Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:19 وَفِىٓ أَمْوَٰلِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّآئِلِ وَٱلْمَحْرُومِ
51:19 Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:20 وَفِى ٱلْأَرْضِ ءَايَـٰتٌ لِّلْمُوقِنِينَ
51:20 Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:21 وَفِىٓ أَنفُسِكُمْ ۚ أَفَلَا تُبْصِرُونَ
51:21 Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:22 وَفِى ٱلسَّمَآءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ
51:22 Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:23 فَوَرَبِّ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ إِنَّهُۥ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَآ أَنَّكُمْ تَنطِقُونَ
51:23 Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo kweli kuwa nyinyi mnasema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:24 هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَٰهِيمَ ٱلْمُكْرَمِينَ
51:24 Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:25 إِذْ دَخَلُوا۟ عَلَيْهِ فَقَالُوا۟ سَلَـٰمًا ۖ قَالَ سَلَـٰمٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ
51:25 Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu nisio kujueni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:26 فَرَاغَ إِلَىٰٓ أَهْلِهِۦ فَجَآءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ
51:26 Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:27 فَقَرَّبَهُۥٓ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ
51:27 Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:28 فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۖ قَالُوا۟ لَا تَخَفْ ۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَـٰمٍ عَلِيمٍ
51:28 Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria kupata kijana mwenye ilimu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:29 فَأَقْبَلَتِ ٱمْرَأَتُهُۥ فِى صَرَّةٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيمٌ
51:29 Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na kusema: Mimi ni kikongwe na tasa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:30 قَالُوا۟ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ ۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْحَكِيمُ ٱلْعَلِيمُ
51:30 Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mwenye kujua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:31 ۞ قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا ٱلْمُرْسَلُونَ
51:31 AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:32 قَالُوٓا۟ إِنَّآ أُرْسِلْنَآ إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ
51:32 Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:33 لِنُرْسِلَ عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن طِينٍ
51:33 Tuwatupie mawe ya udongo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:34 مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلْمُسْرِفِينَ
51:34 Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:35 فَأَخْرَجْنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ
51:35 Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:36 فَمَا وَجَدْنَا فِيهَا غَيْرَ بَيْتٍ مِّنَ ٱلْمُسْلِمِينَ
51:36 Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:37 وَتَرَكْنَا فِيهَآ ءَايَةً لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ ٱلْعَذَابَ ٱلْأَلِيمَ
51:37 Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:38 وَفِى مُوسَىٰٓ إِذْ أَرْسَلْنَـٰهُ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ بِسُلْطَـٰنٍ مُّبِينٍ
51:38 Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:39 فَتَوَلَّىٰ بِرُكْنِهِۦ وَقَالَ سَـٰحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ
51:39 Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:40 فَأَخَذْنَـٰهُ وَجُنُودَهُۥ فَنَبَذْنَـٰهُمْ فِى ٱلْيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٌ
51:40 Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa kulaumiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:41 وَفِى عَادٍ إِذْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ ٱلرِّيحَ ٱلْعَقِيمَ
51:41 Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa kukata uzazi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:42 مَا تَذَرُ مِن شَىْءٍ أَتَتْ عَلَيْهِ إِلَّا جَعَلَتْهُ كَٱلرَّمِيمِ
51:42 Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya kama kilio nyambuka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:43 وَفِى ثَمُودَ إِذْ قِيلَ لَهُمْ تَمَتَّعُوا۟ حَتَّىٰ حِينٍ
51:43 Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:44 فَعَتَوْا۟ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ فَأَخَذَتْهُمُ ٱلصَّـٰعِقَةُ وَهُمْ يَنظُرُونَ
51:44 Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:45 فَمَا ٱسْتَطَـٰعُوا۟ مِن قِيَامٍ وَمَا كَانُوا۟ مُنتَصِرِينَ
51:45 Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:46 وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَوْمًا فَـٰسِقِينَ
51:46 Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:47 وَٱلسَّمَآءَ بَنَيْنَـٰهَا بِأَيْي۟دٍ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ
51:47 Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio twenye uwezo wa kuzitanua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:48 وَٱلْأَرْضَ فَرَشْنَـٰهَا فَنِعْمَ ٱلْمَـٰهِدُونَ
51:48 Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:49 وَمِن كُلِّ شَىْءٍ خَلَقْنَا زَوْجَيْنِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ
51:49 Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:50 فَفِرُّوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ ۖ إِنِّى لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ
51:50 Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:51 وَلَا تَجْعَلُوا۟ مَعَ ٱللَّهِ إِلَـٰهًا ءَاخَرَ ۖ إِنِّى لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ
51:51 Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:52 كَذَٰلِكَ مَآ أَتَى ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُوا۟ سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ
51:52 Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au mwendawazimu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:53 أَتَوَاصَوْا۟ بِهِۦ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ
51:53 Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:54 فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَمَآ أَنتَ بِمَلُومٍ
51:54 Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:55 وَذَكِّرْ فَإِنَّ ٱلذِّكْرَىٰ تَنفَعُ ٱلْمُؤْمِنِينَ
51:55 Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:56 وَمَا خَلَقْتُ ٱلْجِنَّ وَٱلْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ
51:56 Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:57 مَآ أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَآ أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ
51:57 Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:58 إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلرَّزَّاقُ ذُو ٱلْقُوَّةِ ٱلْمَتِينُ
51:58 Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:59 فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ ذَنُوبًا مِّثْلَ ذَنُوبِ أَصْحَـٰبِهِمْ فَلَا يَسْتَعْجِلُونِ
51:59 Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi wasinihimize. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

51:60 فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِن يَوْمِهِمُ ٱلَّذِى يُوعَدُونَ
51:60 Ole wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)