Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

52 Aţ-Ţūr ٱلطُّور

< Previous   49 Āyah   The Mount      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

52:1 وَٱلطُّورِ
52:1 Naapa kwa mlima wa T'ur, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:2 وَكِتَـٰبٍ مَّسْطُورٍ
52:2 Na Kitabu kilicho andikwa - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:3 فِى رَقٍّ مَّنشُورٍ
52:3 Katika ngozi iliyo kunjuliwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:4 وَٱلْبَيْتِ ٱلْمَعْمُورِ
52:4 Na kwa Nyumba iliyo jengwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:5 وَٱلسَّقْفِ ٱلْمَرْفُوعِ
52:5 Na kwa dari iliyo nyanyuliwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:6 وَٱلْبَحْرِ ٱلْمَسْجُورِ
52:6 Na kwa bahari iliyo jazwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:7 إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ لَوَٰقِعٌ
52:7 Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi hapana shaka itatokea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:8 مَّا لَهُۥ مِن دَافِعٍ
52:8 Hapana wa kuizuia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:9 يَوْمَ تَمُورُ ٱلسَّمَآءُ مَوْرًا
52:9 Siku zitakapo tikisika mbingu kwa mtikiso, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:10 وَتَسِيرُ ٱلْجِبَالُ سَيْرًا
52:10 Na milima iwe inakwenda kwa mwendo mkubwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:11 فَوَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
52:11 Basi ole wao siku hiyo hao wanao kadhibisha, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:12 ٱلَّذِينَ هُمْ فِى خَوْضٍ يَلْعَبُونَ
52:12 Ambao wanacheza katika mambo ya upuuzi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:13 يَوْمَ يُدَعُّونَ إِلَىٰ نَارِ جَهَنَّمَ دَعًّا
52:13 Siku watapo sukumwa kwenye Moto kwa msukumo wa nguvu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:14 هَـٰذِهِ ٱلنَّارُ ٱلَّتِى كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ
52:14 (Waambiwe): Huu ndio ule Moto mlio kuwa mkiukanusha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:15 أَفَسِحْرٌ هَـٰذَآ أَمْ أَنتُمْ لَا تُبْصِرُونَ
52:15 Je! Huu ni uchawi, au hamwoni tu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:16 ٱصْلَوْهَا فَٱصْبِرُوٓا۟ أَوْ لَا تَصْبِرُوا۟ سَوَآءٌ عَلَيْكُمْ ۖ إِنَّمَا تُجْزَوْنَ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
52:16 Uingieni, mkistahamili au msistahamili - ni mamoja kwenu. Hakika mnalipwa kwa mliyo kuwa mkiyatenda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:17 إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى جَنَّـٰتٍ وَنَعِيمٍ
52:17 Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na neema, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:18 فَـٰكِهِينَ بِمَآ ءَاتَىٰهُمْ رَبُّهُمْ وَوَقَىٰهُمْ رَبُّهُمْ عَذَابَ ٱلْجَحِيمِ
52:18 Wakifurahi kwa yale aliyo wapa Mola wao Mlezi. Na Mola wao Mlezi atawalinda na adhabu ya Motoni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:19 كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ هَنِيٓـًٔۢا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
52:19 Kuleni na kunyweni kwa raha kabisa kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyatenda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:20 مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ سُرُرٍ مَّصْفُوفَةٍ ۖ وَزَوَّجْنَـٰهُم بِحُورٍ عِينٍ
52:20 Watakuwa wameegemea juu ya viti vya enzi vilivyo pangwa kwa safu. Na tutawaoza mahuru-l-aini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:21 وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَـٰنٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَآ أَلَتْنَـٰهُم مِّنْ عَمَلِهِم مِّن شَىْءٍ ۚ كُلُّ ٱمْرِئٍۭ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ
52:21 Na walio amini na dhuriya zao wakawafuata kwa Imani tutawakutanisha nao dhuriya zao, na wala hatutawapunja hata kidogo katika vitendo vyao. Kila mtu lazima atapata alicho kichuma. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:22 وَأَمْدَدْنَـٰهُم بِفَـٰكِهَةٍ وَلَحْمٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ
52:22 Na tutawapa matunda, na nyama kama watavyo penda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:23 يَتَنَـٰزَعُونَ فِيهَا كَأْسًا لَّا لَغْوٌ فِيهَا وَلَا تَأْثِيمٌ
52:23 Watapeana humo bilauri zisio na vinywaji vya kuleta maneno ya upuuzi wala dhambi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:24 ۞ وَيَطُوفُ عَلَيْهِمْ غِلْمَانٌ لَّهُمْ كَأَنَّهُمْ لُؤْلُؤٌ مَّكْنُونٌ
52:24 Iwe wanawapitia watumishi wao kama kwamba ni lulu zilizomo katika chaza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:25 وَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَسَآءَلُونَ
52:25 Wataelekeana wakiulizana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:26 قَالُوٓا۟ إِنَّا كُنَّا قَبْلُ فِىٓ أَهْلِنَا مُشْفِقِينَ
52:26 Waseme: Tulikuwa zamani pamoja na ahali zetu tukiogopa; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:27 فَمَنَّ ٱللَّهُ عَلَيْنَا وَوَقَىٰنَا عَذَابَ ٱلسَّمُومِ
52:27 Basi Mwenyezi Mungu akatufanyia hisani na akatulinda na adhabu ya upepo wa Moto. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:28 إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلُ نَدْعُوهُ ۖ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْبَرُّ ٱلرَّحِيمُ
52:28 Hakika sisi zamani tulikuwa tukimwomba Yeye tu. Hakika Yeye ndiye Mwema Mwenye kurehemu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:29 فَذَكِّرْ فَمَآ أَنتَ بِنِعْمَتِ رَبِّكَ بِكَاهِنٍ وَلَا مَجْنُونٍ
52:29 Basi kumbusha! Kwani wewe, kwa neema ya Mola wako Mlezi, si kuhani wala mwendawazimu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:30 أَمْ يَقُولُونَ شَاعِرٌ نَّتَرَبَّصُ بِهِۦ رَيْبَ ٱلْمَنُونِ
52:30 Au wanasema: Huyu ni mtunga mashairi, tunamtarajia kupatilizwa na dahari. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:31 قُلْ تَرَبَّصُوا۟ فَإِنِّى مَعَكُم مِّنَ ٱلْمُتَرَبِّصِينَ
52:31 Sema: Tarajieni, na mimi pia ni pamoja nanyi katika kutarajia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:32 أَمْ تَأْمُرُهُمْ أَحْلَـٰمُهُم بِهَـٰذَآ ۚ أَمْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ
52:32 Au hizo akili zao ndio zinawaamrisha haya, au wao basi ni watu majeuri tu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:33 أَمْ يَقُولُونَ تَقَوَّلَهُۥ ۚ بَل لَّا يُؤْمِنُونَ
52:33 Au ndio wanasema: Ameitunga hii! Bali basi tu hawaamini! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:34 فَلْيَأْتُوا۟ بِحَدِيثٍ مِّثْلِهِۦٓ إِن كَانُوا۟ صَـٰدِقِينَ
52:34 Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:35 أَمْ خُلِقُوا۟ مِنْ غَيْرِ شَىْءٍ أَمْ هُمُ ٱلْخَـٰلِقُونَ
52:35 Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:36 أَمْ خَلَقُوا۟ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ ۚ بَل لَّا يُوقِنُونَ
52:36 Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:37 أَمْ عِندَهُمْ خَزَآئِنُ رَبِّكَ أَمْ هُمُ ٱلْمُصَۣيْطِرُونَ
52:37 Au wanazo khazina za Mola wako Mlezi au wao ndio wenye madaraka? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:38 أَمْ لَهُمْ سُلَّمٌ يَسْتَمِعُونَ فِيهِ ۖ فَلْيَأْتِ مُسْتَمِعُهُم بِسُلْطَـٰنٍ مُّبِينٍ
52:38 Au wanazo ngazi za kusikilizia? Basi huyo msikilizaji wao na alete hoja ilio wazi! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:39 أَمْ لَهُ ٱلْبَنَـٰتُ وَلَكُمُ ٱلْبَنُونَ
52:39 Au Yeye Mwenyezi Mungu ana wasichana, na nyinyi ndio mna wavulana? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:40 أَمْ تَسْـَٔلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ
52:40 Au wewe unawaomba ujira, na kwa hivyo ndio wanaelemewa na uzito wa gharama? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:41 أَمْ عِندَهُمُ ٱلْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ
52:41 Au wanayo ilimu ya ghaibu, nao wameandika? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:42 أَمْ يُرِيدُونَ كَيْدًا ۖ فَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ هُمُ ٱلْمَكِيدُونَ
52:42 Au wanataka kufanya vitimbi tu? Lakini hao walio kufuru ndio watakao tegeka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:43 أَمْ لَهُمْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ ٱللَّهِ ۚ سُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ
52:43 Au wanae mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu? Subhanallah! Ametaksika Mwenyezi Mungu na hao wanao washirikisha naye. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:44 وَإِن يَرَوْا۟ كِسْفًا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ سَاقِطًا يَقُولُوا۟ سَحَابٌ مَّرْكُومٌ
52:44 Na hata wange ona pande linatoka mbinguni linaanguka wange sema: Ni mawingu yaliyo bebana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:45 فَذَرْهُمْ حَتَّىٰ يُلَـٰقُوا۟ يَوْمَهُمُ ٱلَّذِى فِيهِ يُصْعَقُونَ
52:45 Basi waache mpaka wakutane na siku yao watakapo hilikishwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:46 يَوْمَ لَا يُغْنِى عَنْهُمْ كَيْدُهُمْ شَيْـًٔا وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ
52:46 Siku ambayo hila zao hazitawafaa hata kidogo, wala wao hawatanusuriwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:47 وَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا۟ عَذَابًا دُونَ ذَٰلِكَ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
52:47 Na hakika walio dhulumu watapata adhabu nyengine isiyo kuwa hii, lakini wengi wao hawajui. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:48 وَٱصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ فَإِنَّكَ بِأَعْيُنِنَا ۖ وَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ حِينَ تَقُومُ
52:48 Na ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi. Kwani wewe hakika uko mbele ya macho yetu, na mtakase kwa kumsifu Mola wako Mlezi unapo simama, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

52:49 وَمِنَ ٱلَّيْلِ فَسَبِّحْهُ وَإِدْبَـٰرَ ٱلنُّجُومِ
52:49 Na usiku pia mtakase, na zinapo kuchwa nyota. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)