Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

69 Al-Ĥāqqah ٱلْحَاقَّة

< Previous   52 Āyah   The Reality      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

69:1 ٱلْحَآقَّةُ
69:1 Tukio la haki. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:2 مَا ٱلْحَآقَّةُ
69:2 Nini hilo Tukio la haki? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:3 وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا ٱلْحَآقَّةُ
69:3 Na nini kitakujuulisha nini hilo Tukio la haki? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:4 كَذَّبَتْ ثَمُودُ وَعَادٌۢ بِٱلْقَارِعَةِ
69:4 Thamudi na A'di waliukadhibisha Msiba unao situsha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:5 فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهْلِكُوا۟ بِٱلطَّاغِيَةِ
69:5 Basi Thamudi waliangamizwa kwa balaa kubwa mno. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:6 وَأَمَّا عَادٌ فَأُهْلِكُوا۟ بِرِيحٍ صَرْصَرٍ عَاتِيَةٍ
69:6 Na ama A'di waliangamizwa kwa upepo mkali usio zuilika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:7 سَخَّرَهَا عَلَيْهِمْ سَبْعَ لَيَالٍ وَثَمَـٰنِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومًا فَتَرَى ٱلْقَوْمَ فِيهَا صَرْعَىٰ كَأَنَّهُمْ أَعْجَازُ نَخْلٍ خَاوِيَةٍ
69:7 Alio wapelekea masiku saba, na siku nane, mfululizo bila ya kusita. Utaona watu wamepinduka kama kwamba ni magongo ya mitende yalio wazi ndani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:8 فَهَلْ تَرَىٰ لَهُم مِّنۢ بَاقِيَةٍ
69:8 Basi je! Unamwona mmoja wao aliye baki? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:9 وَجَآءَ فِرْعَوْنُ وَمَن قَبْلَهُۥ وَٱلْمُؤْتَفِكَـٰتُ بِٱلْخَاطِئَةِ
69:9 Na Firauni na walio mtangulia, na miji iliyo pinduliwa chini juu, walileta khatia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:10 فَعَصَوْا۟ رَسُولَ رَبِّهِمْ فَأَخَذَهُمْ أَخْذَةً رَّابِيَةً
69:10 Wakamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato ulio zidi nguvu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:11 إِنَّا لَمَّا طَغَا ٱلْمَآءُ حَمَلْنَـٰكُمْ فِى ٱلْجَارِيَةِ
69:11 Maji yalipo furika Sisi tulikupandisheni katika safina, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:12 لِنَجْعَلَهَا لَكُمْ تَذْكِرَةً وَتَعِيَهَآ أُذُنٌ وَٰعِيَةٌ
69:12 Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalo sikia liyahifadhi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:13 فَإِذَا نُفِخَ فِى ٱلصُّورِ نَفْخَةٌ وَٰحِدَةٌ
69:13 Na litapo pulizwa barugumu mpulizo mmoja tu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:14 وَحُمِلَتِ ٱلْأَرْضُ وَٱلْجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةً وَٰحِدَةً
69:14 Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:15 فَيَوْمَئِذٍ وَقَعَتِ ٱلْوَاقِعَةُ
69:15 Siku hiyo ndio Tukio litatukia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:16 وَٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَهِىَ يَوْمَئِذٍ وَاهِيَةٌ
69:16 Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:17 وَٱلْمَلَكُ عَلَىٰٓ أَرْجَآئِهَا ۚ وَيَحْمِلُ عَرْشَ رَبِّكَ فَوْقَهُمْ يَوْمَئِذٍ ثَمَـٰنِيَةٌ
69:17 Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:18 يَوْمَئِذٍ تُعْرَضُونَ لَا تَخْفَىٰ مِنكُمْ خَافِيَةٌ
69:18 Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:19 فَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَيَقُولُ هَآؤُمُ ٱقْرَءُوا۟ كِتَـٰبِيَهْ
69:19 Basi ama atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:20 إِنِّى ظَنَنتُ أَنِّى مُلَـٰقٍ حِسَابِيَهْ
69:20 Hakika nalijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:21 فَهُوَ فِى عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ
69:21 Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:22 فِى جَنَّةٍ عَالِيَةٍ
69:22 Katika Bustani ya juu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:23 قُطُوفُهَا دَانِيَةٌ
69:23 Matunda yake yakaribu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:24 كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ هَنِيٓـًٔۢا بِمَآ أَسْلَفْتُمْ فِى ٱلْأَيَّامِ ٱلْخَالِيَةِ
69:24 Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyo tanguliza katika siku zilizo pita. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:25 وَأَمَّا مَنْ أُوتِىَ كِتَـٰبَهُۥ بِشِمَالِهِۦ فَيَقُولُ يَـٰلَيْتَنِى لَمْ أُوتَ كِتَـٰبِيَهْ
69:25 Na ama atakaye pewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingeli pewa kitabu changu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:26 وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيَهْ
69:26 Wala nisingeli jua nini hisabu yangu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:27 يَـٰلَيْتَهَا كَانَتِ ٱلْقَاضِيَةَ
69:27 Laiti mauti ndiyo yangeli kuwa ya kunimaliza kabisa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:28 مَآ أَغْنَىٰ عَنِّى مَالِيَهْ ۜ
69:28 Mali yangu hayakunifaa kitu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:29 هَلَكَ عَنِّى سُلْطَـٰنِيَهْ
69:29 Madaraka yangu yamenipotea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:30 خُذُوهُ فَغُلُّوهُ
69:30 (Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:31 ثُمَّ ٱلْجَحِيمَ صَلُّوهُ
69:31 Kisha mtupeni Motoni! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:32 ثُمَّ فِى سِلْسِلَةٍ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعًا فَٱسْلُكُوهُ
69:32 Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabiini! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:33 إِنَّهُۥ كَانَ لَا يُؤْمِنُ بِٱللَّهِ ٱلْعَظِيمِ
69:33 Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:34 وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلْمِسْكِينِ
69:34 Wala hahimizi kulisha masikini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:35 فَلَيْسَ لَهُ ٱلْيَوْمَ هَـٰهُنَا حَمِيمٌ
69:35 Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:36 وَلَا طَعَامٌ إِلَّا مِنْ غِسْلِينٍ
69:36 Wala hana chakula ila usaha wa watu wa Motoni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:37 لَّا يَأْكُلُهُۥٓ إِلَّا ٱلْخَـٰطِـُٔونَ
69:37 Chakula hicho hawakili ila wakosefu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:38 فَلَآ أُقْسِمُ بِمَا تُبْصِرُونَ
69:38 Basi naapa kwa mnavyo viona, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:39 وَمَا لَا تُبْصِرُونَ
69:39 Na msivyo viona, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:40 إِنَّهُۥ لَقَوْلُ رَسُولٍ كَرِيمٍ
69:40 Kwa hakika hii ni kauli iliyo letwa na Mjumbe mwenye hishima. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:41 وَمَا هُوَ بِقَوْلِ شَاعِرٍ ۚ قَلِيلًا مَّا تُؤْمِنُونَ
69:41 Wala si kauli ya mtunga mashairi. Ni machache sana mnayo yaamini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:42 وَلَا بِقَوْلِ كَاهِنٍ ۚ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ
69:42 Wala si kauli ya kuhani. Ni machache mnayo yakumbuka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:43 تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
69:43 Ni uteremsho utokao kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:44 وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ ٱلْأَقَاوِيلِ
69:44 Na lau kama angeli tuzulia baadhi ya maneno tu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:45 لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِٱلْيَمِينِ
69:45 Bila ya shaka tungeli mshika kwa mkono wa kulia, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:46 ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ ٱلْوَتِينَ
69:46 Kisha kwa hakika tungeli mkata mshipa mkubwa wa moyo! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:47 فَمَا مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَـٰجِزِينَ
69:47 Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeli weza kutuzuia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:48 وَإِنَّهُۥ لَتَذْكِرَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ
69:48 Kwa hakika hii ni mawaidha kwa wachamngu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:49 وَإِنَّا لَنَعْلَمُ أَنَّ مِنكُم مُّكَذِّبِينَ
69:49 Na hakika Sisi bila ya shaka tunajua kwamba miongoni mwenu wapo wanao kadhibisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:50 وَإِنَّهُۥ لَحَسْرَةٌ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ
69:50 Na hakika bila ya shaka itakuwa ni majuto kwa wanao kataa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:51 وَإِنَّهُۥ لَحَقُّ ٱلْيَقِينِ
69:51 Na hakika hii bila ya shaka ni haki ya yakini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

69:52 فَسَبِّحْ بِٱسْمِ رَبِّكَ ٱلْعَظِيمِ
69:52 Basi litakase jina la Mola wako Mlezi Mtukufu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)