Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

88 Al-Ghāshiyah ٱلْغَاشِيَة

< Previous   26 Āyah   The Overwhelming      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

88:1 هَلْ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلْغَـٰشِيَةِ
88:1 Je! Imekufikia khabari ya msiba wa kufudikiza? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:2 وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَـٰشِعَةٌ
88:2 Siku hiyo nyuso zitainama, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:3 عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ
88:3 Zikifanya kazi, nazo taabani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:4 تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً
88:4 Ziingie katika Moto unao waka - - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:5 تُسْقَىٰ مِنْ عَيْنٍ ءَانِيَةٍ
88:5 Zikinyweshwa kutoka chemchem inayo chemka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:6 لَّيْسَ لَهُمْ طَعَامٌ إِلَّا مِن ضَرِيعٍ
88:6 Hawatakuwa na chakula isipo kuwa kichungu chenye miba. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:7 لَّا يُسْمِنُ وَلَا يُغْنِى مِن جُوعٍ
88:7 Hakinenepeshi wala hakiondoi njaa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:8 وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ نَّاعِمَةٌ
88:8 Siku hiyo nyuso nyengine zitakuwa kunjufu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:9 لِّسَعْيِهَا رَاضِيَةٌ
88:9 Zitakuwa radhi kwa juhudi yao, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:10 فِى جَنَّةٍ عَالِيَةٍ
88:10 Katika Bustani ya juu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:11 لَّا تَسْمَعُ فِيهَا لَـٰغِيَةً
88:11 Hawatasikia humo upuuzi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:12 فِيهَا عَيْنٌ جَارِيَةٌ
88:12 Humo imo chemchem inayo miminika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:13 فِيهَا سُرُرٌ مَّرْفُوعَةٌ
88:13 Humo vimo viti vilivyo nyanyuliwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:14 وَأَكْوَابٌ مَّوْضُوعَةٌ
88:14 Na bilauri zilizo pangwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:15 وَنَمَارِقُ مَصْفُوفَةٌ
88:15 Na matakia safu safu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:16 وَزَرَابِىُّ مَبْثُوثَةٌ
88:16 Na mazulia yaliyo tandikwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:17 أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى ٱلْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ
88:17 Je! Hawamtazami ngamia jinsi alivyo umbwa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:18 وَإِلَى ٱلسَّمَآءِ كَيْفَ رُفِعَتْ
88:18 Na mbingu jinsi ilivyo inuliwa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:19 وَإِلَى ٱلْجِبَالِ كَيْفَ نُصِبَتْ
88:19 Na milima jinsi ilivyo thibitishwa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:20 وَإِلَى ٱلْأَرْضِ كَيْفَ سُطِحَتْ
88:20 Na ardhi jinsi ilivyo tandazwa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:21 فَذَكِّرْ إِنَّمَآ أَنتَ مُذَكِّرٌ
88:21 Basi kumbusha! Hakika wewe ni Mkumbushaji. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:22 لَّسْتَ عَلَيْهِم بِمُصَيْطِرٍ
88:22 Wewe si mwenye kuwatawalia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:23 إِلَّا مَن تَوَلَّىٰ وَكَفَرَ
88:23 Lakini anaye rudi nyuma na kukataa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:24 فَيُعَذِّبُهُ ٱللَّهُ ٱلْعَذَابَ ٱلْأَكْبَرَ
88:24 Basi Mwenyezi Mungu atamuadhibu kwa adhabu iliyo kubwa kabisa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:25 إِنَّ إِلَيْنَآ إِيَابَهُمْ
88:25 Hakika ni kwetu Sisi ndio marejeo yao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

88:26 ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُم
88:26 Kisha hakika ni juu yetu Sisi hisabu yao! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)