Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

100 Al-`Ādiyāt ٱلْعَادِيَات

< Previous   11 Āyah   The Courser      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

100:1 وَٱلْعَـٰدِيَـٰتِ ضَبْحًا
100:1 Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

100:2 فَٱلْمُورِيَـٰتِ قَدْحًا
100:2 Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

100:3 فَٱلْمُغِيرَٰتِ صُبْحًا
100:3 Wakishambulia wakati wa asubuhi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

100:4 فَأَثَرْنَ بِهِۦ نَقْعًا
100:4 Huku wakitimua vumbi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

100:5 فَوَسَطْنَ بِهِۦ جَمْعًا
100:5 Na wakijitoma kati ya kundi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

100:6 إِنَّ ٱلْإِنسَـٰنَ لِرَبِّهِۦ لَكَنُودٌ
100:6 Hakika mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

100:7 وَإِنَّهُۥ عَلَىٰ ذَٰلِكَ لَشَهِيدٌ
100:7 Na hakika yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

100:8 وَإِنَّهُۥ لِحُبِّ ٱلْخَيْرِ لَشَدِيدٌ
100:8 Naye hakika bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

100:9 ۞ أَفَلَا يَعْلَمُ إِذَا بُعْثِرَ مَا فِى ٱلْقُبُورِ
100:9 Kwani hajui watakapo fufuliwa waliomo makaburini? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

100:10 وَحُصِّلَ مَا فِى ٱلصُّدُورِ
100:10 Na yakakusanywa yaliomo vifuani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

100:11 إِنَّ رَبَّهُم بِهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّخَبِيرٌۢ
100:11 Kuwa hakika Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)