Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

74 Al-Muddaththir ٱلْمُدَّثِّر

< Previous   56 Āyah   The Cloaked One      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

74:1 يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْمُدَّثِّرُ
74:1 Ewe uliye jigubika! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:2 قُمْ فَأَنذِرْ
74:2 Simama uonye! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:3 وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ
74:3 Na Mola wako Mlezi mtukuze! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:4 وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ
74:4 Na nguo zako, zisafishe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:5 وَٱلرُّجْزَ فَٱهْجُرْ
74:5 Na yaliyo machafu yahame! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:6 وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ
74:6 Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:7 وَلِرَبِّكَ فَٱصْبِرْ
74:7 Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:8 فَإِذَا نُقِرَ فِى ٱلنَّاقُورِ
74:8 Basi litapo pulizwa barugumu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:9 فَذَٰلِكَ يَوْمَئِذٍ يَوْمٌ عَسِيرٌ
74:9 Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:10 عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ غَيْرُ يَسِيرٍ
74:10 Kwa makafiri haitakuwa nyepesi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:11 ذَرْنِى وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا
74:11 Niache peke yangu na niliye muumba; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:12 وَجَعَلْتُ لَهُۥ مَالًا مَّمْدُودًا
74:12 Na nikamjaalia awe na mali mengi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:13 وَبَنِينَ شُهُودًا
74:13 Na wana wanao onekana, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:14 وَمَهَّدتُّ لَهُۥ تَمْهِيدًا
74:14 Na nikamtgenezea mambo vizuri kabisa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:15 ثُمَّ يَطْمَعُ أَنْ أَزِيدَ
74:15 Kisha anatumai nimzidishie! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:16 كَلَّآ ۖ إِنَّهُۥ كَانَ لِـَٔايَـٰتِنَا عَنِيدًا
74:16 Hasha! Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:17 سَأُرْهِقُهُۥ صَعُودًا
74:17 Nitamtesa kwa mateso yasio wezekana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:18 إِنَّهُۥ فَكَّرَ وَقَدَّرَ
74:18 Kwani hakika yeye alifikiri na akapima. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:19 فَقُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ
74:19 Basi ameangamia! Vipi alivyo pima! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:20 ثُمَّ قُتِلَ كَيْفَ قَدَّرَ
74:20 Tena ameangamia! Vipi alivyo pima! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:21 ثُمَّ نَظَرَ
74:21 Kisha akatazama, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:22 ثُمَّ عَبَسَ وَبَسَرَ
74:22 Kisha akakunja kipaji, na akanuna. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:23 ثُمَّ أَدْبَرَ وَٱسْتَكْبَرَ
74:23 Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:24 فَقَالَ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ يُؤْثَرُ
74:24 Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio nukuliwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:25 إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا قَوْلُ ٱلْبَشَرِ
74:25 Haya si chochote ila kauli ya binaadamu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:26 سَأُصْلِيهِ سَقَرَ
74:26 Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:27 وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا سَقَرُ
74:27 Na nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:28 لَا تُبْقِى وَلَا تَذَرُ
74:28 Haubakishi wala hausazi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:29 لَوَّاحَةٌ لِّلْبَشَرِ
74:29 Unababua ngozi iwe nyeusi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:30 عَلَيْهَا تِسْعَةَ عَشَرَ
74:30 Juu yake wapo kumi na tisa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:31 وَمَا جَعَلْنَآ أَصْحَـٰبَ ٱلنَّارِ إِلَّا مَلَـٰٓئِكَةً ۙ وَمَا جَعَلْنَا عِدَّتَهُمْ إِلَّا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لِيَسْتَيْقِنَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ وَيَزْدَادَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِيمَـٰنًا ۙ وَلَا يَرْتَابَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْكِتَـٰبَ وَٱلْمُؤْمِنُونَ ۙ وَلِيَقُولَ ٱلَّذِينَ فِى قُلُوبِهِم مَّرَضٌ وَٱلْكَـٰفِرُونَ مَاذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِهَـٰذَا مَثَلًا ۚ كَذَٰلِكَ يُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَهْدِى مَن يَشَآءُ ۚ وَمَا يَعْلَمُ جُنُودَ رَبِّكَ إِلَّا هُوَ ۚ وَمَا هِىَ إِلَّا ذِكْرَىٰ لِلْبَشَرِ
74:31 Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika, wala hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha walio kufuru, wapate kuwa na yakini walio pewa Kitabu, na wazidi Imani wale walio amini, wala wasiwe na shaka walio pewa Kitabu na Waumini, na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndio kama hivyo Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye. Na hapana yeyote anaye jua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote ila ni ukumbusho kwa binaadamu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:32 كَلَّا وَٱلْقَمَرِ
74:32 Hasha! Naapa kwa mwezi! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:33 وَٱلَّيْلِ إِذْ أَدْبَرَ
74:33 Na kwa usiku unapo kucha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:34 وَٱلصُّبْحِ إِذَآ أَسْفَرَ
74:34 Na kwa asubuhi inapo pambazuka! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:35 إِنَّهَا لَإِحْدَى ٱلْكُبَرِ
74:35 Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:36 نَذِيرًا لِّلْبَشَرِ
74:36 Ni onyo kwa binaadamu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:37 لِمَن شَآءَ مِنكُمْ أَن يَتَقَدَّمَ أَوْ يَتَأَخَّرَ
74:37 Kwa anaye taka miongoni mwenu kutangulia au kuchelewa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:38 كُلُّ نَفْسٍۭ بِمَا كَسَبَتْ رَهِينَةٌ
74:38 Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyo yachuma. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:39 إِلَّآ أَصْحَـٰبَ ٱلْيَمِينِ
74:39 Isipo kuwa watu wa kuliani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:40 فِى جَنَّـٰتٍ يَتَسَآءَلُونَ
74:40 Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:41 عَنِ ٱلْمُجْرِمِينَ
74:41 Khabari za wakosefu: - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:42 مَا سَلَكَكُمْ فِى سَقَرَ
74:42 Ni nini kilicho kupelekeni Motoni? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:43 قَالُوا۟ لَمْ نَكُ مِنَ ٱلْمُصَلِّينَ
74:43 Waseme: Hatukuwa miongoni walio kuwa wakisali. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:44 وَلَمْ نَكُ نُطْعِمُ ٱلْمِسْكِينَ
74:44 Wala hatukuwa tukiwalisha masikini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:45 وَكُنَّا نَخُوضُ مَعَ ٱلْخَآئِضِينَ
74:45 Na tulikuwa tukizama pamoja na walio zama katika maovu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:46 وَكُنَّا نُكَذِّبُ بِيَوْمِ ٱلدِّينِ
74:46 Na tulikuwa tukiikanusha siku ya malipo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:47 حَتَّىٰٓ أَتَىٰنَا ٱلْيَقِينُ
74:47 Mpaka yakini ilipo tufikia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:48 فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَـٰعَةُ ٱلشَّـٰفِعِينَ
74:48 Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:49 فَمَا لَهُمْ عَنِ ٱلتَّذْكِرَةِ مُعْرِضِينَ
74:49 Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:50 كَأَنَّهُمْ حُمُرٌ مُّسْتَنفِرَةٌ
74:50 Kama kwamba wao ni mapunda walio timuliwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:51 فَرَّتْ مِن قَسْوَرَةٍۭ
74:51 Wanao mkimbia simba! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:52 بَلْ يُرِيدُ كُلُّ ٱمْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُؤْتَىٰ صُحُفًا مُّنَشَّرَةً
74:52 Ati kila mmoja katika wao anataka apewe nyaraka zilizo funuliwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:53 كَلَّا ۖ بَل لَّا يَخَافُونَ ٱلْـَٔاخِرَةَ
74:53 Hasha! Kwani wao hawaiogopi Akhera? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:54 كَلَّآ إِنَّهُۥ تَذْكِرَةٌ
74:54 Hasha! Kwa hakika huu ni ukumbusho! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:55 فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ
74:55 Basi anaye taka atakumbuka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

74:56 وَمَا يَذْكُرُونَ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ ۚ هُوَ أَهْلُ ٱلتَّقْوَىٰ وَأَهْلُ ٱلْمَغْفِرَةِ
74:56 Na hawatakumbuka isipo kuwa Mwenyezi Mungu atake. Uchamngu ni kwake Yeye, na msamaha ni wake Yeye. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)