Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

55 Ar-Raĥmān ٱلرَّحْمَٰن

< Previous   78 Āyah   The Beneficent      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

55:1 ٱلرَّحْمَـٰنُ
55:1 Arrah'man, Mwingi wa Rehema - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:2 عَلَّمَ ٱلْقُرْءَانَ
55:2 Amefundisha Qur'ani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:3 خَلَقَ ٱلْإِنسَـٰنَ
55:3 Amemuumba mwanaadamu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:4 عَلَّمَهُ ٱلْبَيَانَ
55:4 Akamfundisha kubaini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:5 ٱلشَّمْسُ وَٱلْقَمَرُ بِحُسْبَانٍ
55:5 Jua na mwezi huenda kwa hisabu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:6 وَٱلنَّجْمُ وَٱلشَّجَرُ يَسْجُدَانِ
55:6 Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:7 وَٱلسَّمَآءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ ٱلْمِيزَانَ
55:7 Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:8 أَلَّا تَطْغَوْا۟ فِى ٱلْمِيزَانِ
55:8 Ili msidhulumu katika mizani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:9 وَأَقِيمُوا۟ ٱلْوَزْنَ بِٱلْقِسْطِ وَلَا تُخْسِرُوا۟ ٱلْمِيزَانَ
55:9 Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:10 وَٱلْأَرْضَ وَضَعَهَا لِلْأَنَامِ
55:10 Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:11 فِيهَا فَـٰكِهَةٌ وَٱلنَّخْلُ ذَاتُ ٱلْأَكْمَامِ
55:11 Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:12 وَٱلْحَبُّ ذُو ٱلْعَصْفِ وَٱلرَّيْحَانُ
55:12 Na nafaka zenye makapi, na rehani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:13 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:13 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:14 خَلَقَ ٱلْإِنسَـٰنَ مِن صَلْصَـٰلٍ كَٱلْفَخَّارِ
55:14 Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo.. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:15 وَخَلَقَ ٱلْجَآنَّ مِن مَّارِجٍ مِّن نَّارٍ
55:15 Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:16 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:16 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:17 رَبُّ ٱلْمَشْرِقَيْنِ وَرَبُّ ٱلْمَغْرِبَيْنِ
55:17 Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:18 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:18 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:19 مَرَجَ ٱلْبَحْرَيْنِ يَلْتَقِيَانِ
55:19 Anaziendesha bahari mbili zikutane; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:20 بَيْنَهُمَا بَرْزَخٌ لَّا يَبْغِيَانِ
55:20 Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:21 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:21 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:22 يَخْرُجُ مِنْهُمَا ٱللُّؤْلُؤُ وَٱلْمَرْجَانُ
55:22 Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:23 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:23 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:24 وَلَهُ ٱلْجَوَارِ ٱلْمُنشَـَٔاتُ فِى ٱلْبَحْرِ كَٱلْأَعْلَـٰمِ
55:24 Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa kama vilima. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:25 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:25 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:26 كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ
55:26 Kila kilioko juu yake kitatoweka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:27 وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ ذُو ٱلْجَلَـٰلِ وَٱلْإِكْرَامِ
55:27 Na atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:28 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:28 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:29 يَسْـَٔلُهُۥ مَن فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ ۚ كُلَّ يَوْمٍ هُوَ فِى شَأْنٍ
55:29 Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika mambo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:30 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:30 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:31 سَنَفْرُغُ لَكُمْ أَيُّهَ ٱلثَّقَلَانِ
55:31 Tutakuhisabuni enyi makundi mawili. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:32 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:32 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:33 يَـٰمَعْشَرَ ٱلْجِنِّ وَٱلْإِنسِ إِنِ ٱسْتَطَعْتُمْ أَن تَنفُذُوا۟ مِنْ أَقْطَارِ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ فَٱنفُذُوا۟ ۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلْطَـٰنٍ
55:33 Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:34 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:34 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:35 يُرْسَلُ عَلَيْكُمَا شُوَاظٌ مِّن نَّارٍ وَنُحَاسٌ فَلَا تَنتَصِرَانِ
55:35 Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:36 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:36 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:37 فَإِذَا ٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتْ وَرْدَةً كَٱلدِّهَانِ
55:37 Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:38 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:38 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:39 فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُسْـَٔلُ عَن ذَنۢبِهِۦٓ إِنسٌ وَلَا جَآنٌّ
55:39 Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:40 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:40 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:41 يُعْرَفُ ٱلْمُجْرِمُونَ بِسِيمَـٰهُمْ فَيُؤْخَذُ بِٱلنَّوَٰصِى وَٱلْأَقْدَامِ
55:41 Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa kwa nywele zao za utosini na kwa miguu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:42 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:42 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:43 هَـٰذِهِۦ جَهَنَّمُ ٱلَّتِى يُكَذِّبُ بِهَا ٱلْمُجْرِمُونَ
55:43 Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:44 يَطُوفُونَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ حَمِيمٍ ءَانٍ
55:44 Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto yanayo chemka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:45 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:45 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:46 وَلِمَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ جَنَّتَانِ
55:46 Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi atapata Bustani mbili. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:47 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:47 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:48 ذَوَاتَآ أَفْنَانٍ
55:48 Bustani zenye matawi yaliyo tanda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:49 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:49 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:50 فِيهِمَا عَيْنَانِ تَجْرِيَانِ
55:50 Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:51 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:51 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:52 فِيهِمَا مِن كُلِّ فَـٰكِهَةٍ زَوْجَانِ
55:52 Humo katika kila matunda zimo namna mbili. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:53 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:53 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:54 مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ فُرُشٍۭ بَطَآئِنُهَا مِنْ إِسْتَبْرَقٍ ۚ وَجَنَى ٱلْجَنَّتَيْنِ دَانٍ
55:54 Wawe wameegemea matandiko yenye bit'ana ya hariri nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:55 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:55 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:56 فِيهِنَّ قَـٰصِرَٰتُ ٱلطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَآنٌّ
55:56 Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao; hajawagusa mtu kabla yao wala jini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:57 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:57 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:58 كَأَنَّهُنَّ ٱلْيَاقُوتُ وَٱلْمَرْجَانُ
55:58 Kama kwamba wao ni yakuti na marijani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:59 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:59 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:60 هَلْ جَزَآءُ ٱلْإِحْسَـٰنِ إِلَّا ٱلْإِحْسَـٰنُ
55:60 Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:61 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:61 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:62 وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ
55:62 Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:63 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:63 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:64 مُدْهَآمَّتَانِ
55:64 Za kijani kibivu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:65 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:65 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:66 فِيهِمَا عَيْنَانِ نَضَّاخَتَانِ
55:66 Na chemchem mbili zinazo furika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:67 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:67 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:68 فِيهِمَا فَـٰكِهَةٌ وَنَخْلٌ وَرُمَّانٌ
55:68 Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:69 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:69 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:70 فِيهِنَّ خَيْرَٰتٌ حِسَانٌ
55:70 Humo wamo wanawake wema wazuri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:71 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:71 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:72 حُورٌ مَّقْصُورَٰتٌ فِى ٱلْخِيَامِ
55:72 Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:73 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:73 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:74 لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَآنٌّ
55:74 Hajawagusa mtu wala jini kabla yao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:75 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:75 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:76 مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ رَفْرَفٍ خُضْرٍ وَعَبْقَرِىٍّ حِسَانٍ
55:76 Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:77 فَبِأَىِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
55:77 Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

55:78 تَبَـٰرَكَ ٱسْمُ رَبِّكَ ذِى ٱلْجَلَـٰلِ وَٱلْإِكْرَامِ
55:78 Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)