Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

68 Al-Qalam ٱلْقَلَم

< Previous   52 Āyah   The Pen      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

68:1 نٓ ۚ وَٱلْقَلَمِ وَمَا يَسْطُرُونَ
68:1 Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:2 مَآ أَنتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِمَجْنُونٍ
68:2 Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:3 وَإِنَّ لَكَ لَأَجْرًا غَيْرَ مَمْنُونٍ
68:3 Na kwa hakika wewe una malipo yasiyo katika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:4 وَإِنَّكَ لَعَلَىٰ خُلُقٍ عَظِيمٍ
68:4 Na hakika wewe una tabia tukufu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:5 فَسَتُبْصِرُ وَيُبْصِرُونَ
68:5 Karibu utaona, na wao wataona, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:6 بِأَييِّكُمُ ٱلْمَفْتُونُ
68:6 Ni nani kati yenu aliye pandwa na wazimu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:7 إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعْلَمُ بِٱلْمُهْتَدِينَ
68:7 Hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye ajuaye zaidi nani aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:8 فَلَا تُطِعِ ٱلْمُكَذِّبِينَ
68:8 Basi usiwat'ii wanao kadhibisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:9 وَدُّوا۟ لَوْ تُدْهِنُ فَيُدْهِنُونَ
68:9 Wanatamani lau unge lainisha ili nao wakulainishie. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:10 وَلَا تُطِعْ كُلَّ حَلَّافٍ مَّهِينٍ
68:10 Wala usimt'ii kila mwingi wa kuapa wa kudharauliwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:11 هَمَّازٍ مَّشَّآءٍۭ بِنَمِيمٍ
68:11 Mtapitapi, apitaye akifitini, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:12 مَّنَّاعٍ لِّلْخَيْرِ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ
68:12 Mwenye kuzuia kheri, dhaalimu, mwingi wa madhambi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:13 عُتُلٍّۭ بَعْدَ ذَٰلِكَ زَنِيمٍ
68:13 Mkavu, na juu ya hayo, mshari, amejipachika tu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:14 أَن كَانَ ذَا مَالٍ وَبَنِينَ
68:14 Ati kwa kuwa ana mali na watoto! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:15 إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ ءَايَـٰتُنَا قَالَ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ
68:15 Anapo somewa Aya zetu, husema: Hizi ni simulizi za uwongo za watu wa zamani! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:16 سَنَسِمُهُۥ عَلَى ٱلْخُرْطُومِ
68:16 Tutamtia kovu juu ya pua yake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:17 إِنَّا بَلَوْنَـٰهُمْ كَمَا بَلَوْنَآ أَصْحَـٰبَ ٱلْجَنَّةِ إِذْ أَقْسَمُوا۟ لَيَصْرِمُنَّهَا مُصْبِحِينَ
68:17 Hakika tumewajaribu hawa kama tulivyo wajaribu wale wenye shamba, walipo apa kwamba watayavuna mazao yake itakapo kuwa asubuhi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:18 وَلَا يَسْتَثْنُونَ
68:18 Wala hawakusema: Mungu akipenda! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:19 فَطَافَ عَلَيْهَا طَآئِفٌ مِّن رَّبِّكَ وَهُمْ نَآئِمُونَ
68:19 Basi lilitokea tukio juu yake kutoka kwa Mola wako Mlezi, nao wamelala! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:20 فَأَصْبَحَتْ كَٱلصَّرِيمِ
68:20 Likawa kama usiku wa giza. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:21 فَتَنَادَوْا۟ مُصْبِحِينَ
68:21 Asubuhi wakaitana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:22 أَنِ ٱغْدُوا۟ عَلَىٰ حَرْثِكُمْ إِن كُنتُمْ صَـٰرِمِينَ
68:22 Ya kwamba nendeni kondeni mwenu ikiwa mnataka kuvuna. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:23 فَٱنطَلَقُوا۟ وَهُمْ يَتَخَـٰفَتُونَ
68:23 Basi walikwenda na huku wakinong'onezana, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:24 أَن لَّا يَدْخُلَنَّهَا ٱلْيَوْمَ عَلَيْكُم مِّسْكِينٌ
68:24 Ya kuwa leo hata masikini mmoja asikuingilieni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:25 وَغَدَوْا۟ عَلَىٰ حَرْدٍ قَـٰدِرِينَ
68:25 Na walikwenda asubuhi, nao wameshikilia azimio hilo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:26 فَلَمَّا رَأَوْهَا قَالُوٓا۟ إِنَّا لَضَآلُّونَ
68:26 Basi walipo liona, wakasema: Hakika tumepotea! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:27 بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ
68:27 Bali tumenyimwa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:28 قَالَ أَوْسَطُهُمْ أَلَمْ أَقُل لَّكُمْ لَوْلَا تُسَبِّحُونَ
68:28 Mbora wao akasema: Sikukwambieni, kwa nini hamumtakasi Mwenyezi Mungu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:29 قَالُوا۟ سُبْحَـٰنَ رَبِّنَآ إِنَّا كُنَّا ظَـٰلِمِينَ
68:29 Wakasema: Ametakasika Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tulikuwa wenye kudhulumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:30 فَأَقْبَلَ بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ يَتَلَـٰوَمُونَ
68:30 Basi wakakabiliana kulaumiana wao kwa wao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:31 قَالُوا۟ يَـٰوَيْلَنَآ إِنَّا كُنَّا طَـٰغِينَ
68:31 Wakasema: Ole wetu! Tulikuwa tumeikiuka mipaka! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:32 عَسَىٰ رَبُّنَآ أَن يُبْدِلَنَا خَيْرًا مِّنْهَآ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا رَٰغِبُونَ
68:32 Asaa Mola wetu Mlezi akatubadilishia lilio bora kuliko hili. Hakika sisi ni wenye kurejea kwa Mola wetu Mlezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:33 كَذَٰلِكَ ٱلْعَذَابُ ۖ وَلَعَذَابُ ٱلْـَٔاخِرَةِ أَكْبَرُ ۚ لَوْ كَانُوا۟ يَعْلَمُونَ
68:33 Namna hivi yanakuwa mateso, na bila ya shaka mateso ya Akhera ni makubwa zaidi, laiti wangeli jua! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:34 إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ
68:34 Hakika wachamngu watakuwa na Bustani za neema kwa Mola wao Mlezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:35 أَفَنَجْعَلُ ٱلْمُسْلِمِينَ كَٱلْمُجْرِمِينَ
68:35 Kwani tutawafanya Waislamu kama wakosefu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:36 مَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ
68:36 Mna nini? Mnahukumu vipi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:37 أَمْ لَكُمْ كِتَـٰبٌ فِيهِ تَدْرُسُونَ
68:37 Au mnacho kitabu ambacho ndani yake mnasoma? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:38 إِنَّ لَكُمْ فِيهِ لَمَا تَخَيَّرُونَ
68:38 Kuwa mtapata humo mnayo yapenda? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:39 أَمْ لَكُمْ أَيْمَـٰنٌ عَلَيْنَا بَـٰلِغَةٌ إِلَىٰ يَوْمِ ٱلْقِيَـٰمَةِ ۙ إِنَّ لَكُمْ لَمَا تَحْكُمُونَ
68:39 Au mnazo ahadi za viapo juu yetu za kufika Siku ya Kiyama ya kuwa hakika mtapata kila mnayo jihukumia? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:40 سَلْهُمْ أَيُّهُم بِذَٰلِكَ زَعِيمٌ
68:40 Waulize: Ni nani miongoni mwao dhamini wa haya? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:41 أَمْ لَهُمْ شُرَكَآءُ فَلْيَأْتُوا۟ بِشُرَكَآئِهِمْ إِن كَانُوا۟ صَـٰدِقِينَ
68:41 Au wanao washirika? Basi wawalete washirika wao wakiwa wanasema kweli. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:42 يَوْمَ يُكْشَفُ عَن سَاقٍ وَيُدْعَوْنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ
68:42 Siku utakapo wekwa wazi mundi, na wataitwa kusujudu, lakini hawataweza, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:43 خَـٰشِعَةً أَبْصَـٰرُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۖ وَقَدْ كَانُوا۟ يُدْعَوْنَ إِلَى ٱلسُّجُودِ وَهُمْ سَـٰلِمُونَ
68:43 Macho yao yatainama chini, fedheha itawafunika. Na hakika walikuwa wakiitwa wasujudu walipo kuwa wazima - - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:44 فَذَرْنِى وَمَن يُكَذِّبُ بِهَـٰذَا ٱلْحَدِيثِ ۖ سَنَسْتَدْرِجُهُم مِّنْ حَيْثُ لَا يَعْلَمُونَ
68:44 Basi niache na wanao kadhibisha maneno haya! Tutawavutia kidogo kidogo kwa mahali wasipo pajua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:45 وَأُمْلِى لَهُمْ ۚ إِنَّ كَيْدِى مَتِينٌ
68:45 Na ninawapururia muhula; hakika hila zangu ni imara. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:46 أَمْ تَسْـَٔلُهُمْ أَجْرًا فَهُم مِّن مَّغْرَمٍ مُّثْقَلُونَ
68:46 Au unawaomba ujira, na wao wanaemewa na gharama hiyo? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:47 أَمْ عِندَهُمُ ٱلْغَيْبُ فَهُمْ يَكْتُبُونَ
68:47 Au iko kwao siri, basi wao wanaiandika? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:48 فَٱصْبِرْ لِحُكْمِ رَبِّكَ وَلَا تَكُن كَصَاحِبِ ٱلْحُوتِ إِذْ نَادَىٰ وَهُوَ مَكْظُومٌ
68:48 Basi ingojee hukumu ya Mola wako Mlezi, wala usiwe kama mmezwa na samaki, alipo nadi naye kazongwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:49 لَّوْلَآ أَن تَدَٰرَكَهُۥ نِعْمَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ لَنُبِذَ بِٱلْعَرَآءِ وَهُوَ مَذْمُومٌ
68:49 Kama isingeli mfikia neema kutoka kwa Mola wake Mlezi, bila ya shaka angeli tupwa ufukweni naye ni mwenye kulaumiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:50 فَٱجْتَبَـٰهُ رَبُّهُۥ فَجَعَلَهُۥ مِنَ ٱلصَّـٰلِحِينَ
68:50 Lakini Mola wake Mlezi alimteua na akamfanya miongoni mwa watu wema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:51 وَإِن يَكَادُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَيُزْلِقُونَكَ بِأَبْصَـٰرِهِمْ لَمَّا سَمِعُوا۟ ٱلذِّكْرَ وَيَقُولُونَ إِنَّهُۥ لَمَجْنُونٌ
68:51 Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

68:52 وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِّلْعَـٰلَمِينَ
68:52 Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)