Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

82 Al-'Infiţār ٱلْإِنْفِطَار

< Previous   19 Āyah   The Cleaving      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

82:1 إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنفَطَرَتْ
82:1 Mbingu itapo chanika, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:2 وَإِذَا ٱلْكَوَاكِبُ ٱنتَثَرَتْ
82:2 Na nyota zitapo tawanyika, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:3 وَإِذَا ٱلْبِحَارُ فُجِّرَتْ
82:3 Na bahari zitakapo pasuliwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:4 وَإِذَا ٱلْقُبُورُ بُعْثِرَتْ
82:4 Na makaburi yatapo fukuliwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:5 عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ
82:5 Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:6 يَـٰٓأَيُّهَا ٱلْإِنسَـٰنُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ ٱلْكَرِيمِ
82:6 Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:7 ٱلَّذِى خَلَقَكَ فَسَوَّىٰكَ فَعَدَلَكَ
82:7 Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:8 فِىٓ أَىِّ صُورَةٍ مَّا شَآءَ رَكَّبَكَ
82:8 Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:9 كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِٱلدِّينِ
82:9 Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:10 وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَـٰفِظِينَ
82:10 Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:11 كِرَامًا كَـٰتِبِينَ
82:11 Waandishi wenye hishima, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:12 يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ
82:12 Wanayajua mnayo yatenda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:13 إِنَّ ٱلْأَبْرَارَ لَفِى نَعِيمٍ
82:13 Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:14 وَإِنَّ ٱلْفُجَّارَ لَفِى جَحِيمٍ
82:14 Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:15 يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ ٱلدِّينِ
82:15 Wataingia humo Siku ya Malipo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:16 وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَآئِبِينَ
82:16 Na hawatoacha kuwamo humo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:17 وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا يَوْمُ ٱلدِّينِ
82:17 Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:18 ثُمَّ مَآ أَدْرَىٰكَ مَا يَوْمُ ٱلدِّينِ
82:18 Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

82:19 يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِّنَفْسٍ شَيْـًٔا ۖ وَٱلْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّهِ
82:19 Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)