Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

70 Al-Ma`ārij ٱلْمَعَارِج

< Previous   44 Āyah   The Ascending Stairways      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

70:1 سَأَلَ سَآئِلٌۢ بِعَذَابٍ وَاقِعٍ
70:1 Muulizaji aliuliza juu ya adhabu itakayo tokea, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:2 لِّلْكَـٰفِرِينَ لَيْسَ لَهُۥ دَافِعٌ
70:2 Kwa makafiri - ambayo hapana awezaye kuizuia - - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:3 مِّنَ ٱللَّهِ ذِى ٱلْمَعَارِجِ
70:3 Kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye mbingu za daraja. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:4 تَعْرُجُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ إِلَيْهِ فِى يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُۥ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ
70:4 Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:5 فَٱصْبِرْ صَبْرًا جَمِيلًا
70:5 Basi subiri kwa subira njema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:6 إِنَّهُمْ يَرَوْنَهُۥ بَعِيدًا
70:6 Hakika wao wanaiona iko mbali, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:7 وَنَرَىٰهُ قَرِيبًا
70:7 Na Sisi tunaiona iko karibu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:8 يَوْمَ تَكُونُ ٱلسَّمَآءُ كَٱلْمُهْلِ
70:8 Siku ambayo mbingu zitakapo kuwa kama maadeni iliyo yayushwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:9 وَتَكُونُ ٱلْجِبَالُ كَٱلْعِهْنِ
70:9 Na milima itakuwa kama sufi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:10 وَلَا يَسْـَٔلُ حَمِيمٌ حَمِيمًا
70:10 Wala jamaa hatamuuliza jamaa yake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:11 يُبَصَّرُونَهُمْ ۚ يَوَدُّ ٱلْمُجْرِمُ لَوْ يَفْتَدِى مِنْ عَذَابِ يَوْمِئِذٍۭ بِبَنِيهِ
70:11 Ijapo kuwa wataonyeshwa waonane. Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:12 وَصَـٰحِبَتِهِۦ وَأَخِيهِ
70:12 Na mkewe, na nduguye, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:13 وَفَصِيلَتِهِ ٱلَّتِى تُـْٔوِيهِ
70:13 Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:14 وَمَن فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا ثُمَّ يُنجِيهِ
70:14 Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:15 كَلَّآ ۖ إِنَّهَا لَظَىٰ
70:15 La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:16 نَزَّاعَةً لِّلشَّوَىٰ
70:16 Unao babua ngozi ya kichwa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:17 تَدْعُوا۟ مَنْ أَدْبَرَ وَتَوَلَّىٰ
70:17 Utamwita kila aliye geuza mgongo na akageuka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:18 وَجَمَعَ فَأَوْعَىٰٓ
70:18 Na akakusanya mali, kisha akayahifadhi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:19 ۞ إِنَّ ٱلْإِنسَـٰنَ خُلِقَ هَلُوعًا
70:19 Hakika mtu ameumbwa na papara. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:20 إِذَا مَسَّهُ ٱلشَّرُّ جَزُوعًا
70:20 Inapo mgusa shari hupapatika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:21 وَإِذَا مَسَّهُ ٱلْخَيْرُ مَنُوعًا
70:21 Na inapo mgusa kheri huizuilia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:22 إِلَّا ٱلْمُصَلِّينَ
70:22 Isipo kuwa wanao sali, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:23 ٱلَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ دَآئِمُونَ
70:23 Ambao wanadumisha Sala zao, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:24 وَٱلَّذِينَ فِىٓ أَمْوَٰلِهِمْ حَقٌّ مَّعْلُومٌ
70:24 Na ambao katika mali yao iko haki maalumu - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:25 لِّلسَّآئِلِ وَٱلْمَحْرُومِ
70:25 Kwa mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:26 وَٱلَّذِينَ يُصَدِّقُونَ بِيَوْمِ ٱلدِّينِ
70:26 Na ambao wanaisadiki Siku ya Malipo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:27 وَٱلَّذِينَ هُم مِّنْ عَذَابِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ
70:27 Na ambao wanaiogopa adhabu itokayo kwa Mola wao Mlezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:28 إِنَّ عَذَابَ رَبِّهِمْ غَيْرُ مَأْمُونٍ
70:28 Hakika adhabu ya Mola wao Mlezi si ya kuaminika nayo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:29 وَٱلَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَـٰفِظُونَ
70:29 Na ambao wanahifadhi tupu zao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:30 إِلَّا عَلَىٰٓ أَزْوَٰجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَـٰنُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ
70:30 Isipo kuwa kwa wake zao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi - - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:31 فَمَنِ ٱبْتَغَىٰ وَرَآءَ ذَٰلِكَ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْعَادُونَ
70:31 Lakini wanao taka kinyume ya haya, basi hao ndio wanao ruka mipaka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:32 وَٱلَّذِينَ هُمْ لِأَمَـٰنَـٰتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَٰعُونَ
70:32 Na ambao wanazichunga amana zao na ahadi zao, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:33 وَٱلَّذِينَ هُم بِشَهَـٰدَٰتِهِمْ قَآئِمُونَ
70:33 Na ambao wanasimama imara katika ushahidi wao, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:34 وَٱلَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ
70:34 Na ambao wanazihifadhi Sala zao. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:35 أُو۟لَـٰٓئِكَ فِى جَنَّـٰتٍ مُّكْرَمُونَ
70:35 Hao ndio watakao hishimiwa Peponi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:36 فَمَالِ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ قِبَلَكَ مُهْطِعِينَ
70:36 Wana nini wale walio kufuru wanakutumbulia macho tu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:37 عَنِ ٱلْيَمِينِ وَعَنِ ٱلشِّمَالِ عِزِينَ
70:37 Makundi kwa makundi upande wa kulia na upande wa kushoto! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:38 أَيَطْمَعُ كُلُّ ٱمْرِئٍ مِّنْهُمْ أَن يُدْخَلَ جَنَّةَ نَعِيمٍ
70:38 Kwani kila mmoja wao anatumai kuingizwa katika Pepo ya neema? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:39 كَلَّآ ۖ إِنَّا خَلَقْنَـٰهُم مِّمَّا يَعْلَمُونَ
70:39 La, hasha! Hakika Sisi tumewaumba kutokana na wanacho kijua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:40 فَلَآ أُقْسِمُ بِرَبِّ ٱلْمَشَـٰرِقِ وَٱلْمَغَـٰرِبِ إِنَّا لَقَـٰدِرُونَ
70:40 Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mashariki zote na magharibi zote kwamba Sisi tunaweza - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:41 عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ خَيْرًا مِّنْهُمْ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ
70:41 Kuwabadili kwa walio bora kuliko wao; na Sisi hatushindwi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:42 فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا۟ وَيَلْعَبُوا۟ حَتَّىٰ يُلَـٰقُوا۟ يَوْمَهُمُ ٱلَّذِى يُوعَدُونَ
70:42 Basi waache wapige porojo na wacheze, mpaka wakutane na siku yao wanayo ahidiwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:43 يَوْمَ يَخْرُجُونَ مِنَ ٱلْأَجْدَاثِ سِرَاعًا كَأَنَّهُمْ إِلَىٰ نُصُبٍ يُوفِضُونَ
70:43 Siku watakapotoka makaburini kwa upesi kama kwamba wanakimbilia mfundo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

70:44 خَـٰشِعَةً أَبْصَـٰرُهُمْ تَرْهَقُهُمْ ذِلَّةٌ ۚ ذَٰلِكَ ٱلْيَوْمُ ٱلَّذِى كَانُوا۟ يُوعَدُونَ
70:44 Macho yao yatainama, fedheha itawafunika. Hiyo ndiyo Siku waliyo kuwa wakiahidiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)