Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

77 Al-Mursalāt ٱلْمُرْسَلَات

< Previous   50 Āyah   The Emissaries      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

77:1 وَٱلْمُرْسَلَـٰتِ عُرْفًا
77:1 Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:2 فَٱلْعَـٰصِفَـٰتِ عَصْفًا
77:2 Na zinazo vuma kwa kasi! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:3 وَٱلنَّـٰشِرَٰتِ نَشْرًا
77:3 Na zikaeneza maeneo yote! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:4 فَٱلْفَـٰرِقَـٰتِ فَرْقًا
77:4 Na zinazo farikisha zikatawanya! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:5 فَٱلْمُلْقِيَـٰتِ ذِكْرًا
77:5 Na zinazo peleka mawaidha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:6 عُذْرًا أَوْ نُذْرًا
77:6 Kwa kuudhuru au kuonya, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:7 إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَٰقِعٌ
77:7 Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:8 فَإِذَا ٱلنُّجُومُ طُمِسَتْ
77:8 Wakati nyota zitakapo futwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:9 وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ فُرِجَتْ
77:9 Na mbingu zitakapo pasuliwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:10 وَإِذَا ٱلْجِبَالُ نُسِفَتْ
77:10 Na milima itakapo peperushwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:11 وَإِذَا ٱلرُّسُلُ أُقِّتَتْ
77:11 Na Mitume watakapo wekewa wakati wao, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:12 لِأَىِّ يَوْمٍ أُجِّلَتْ
77:12 Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:13 لِيَوْمِ ٱلْفَصْلِ
77:13 Kwa siku ya kupambanua! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:14 وَمَآ أَدْرَىٰكَ مَا يَوْمُ ٱلْفَصْلِ
77:14 Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:15 وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
77:15 Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:16 أَلَمْ نُهْلِكِ ٱلْأَوَّلِينَ
77:16 Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:17 ثُمَّ نُتْبِعُهُمُ ٱلْـَٔاخِرِينَ
77:17 Kisha tukawafuatilizia walio fuatia? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:18 كَذَٰلِكَ نَفْعَلُ بِٱلْمُجْرِمِينَ
77:18 Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:19 وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
77:19 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:20 أَلَمْ نَخْلُقكُّم مِّن مَّآءٍ مَّهِينٍ
77:20 Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:21 فَجَعَلْنَـٰهُ فِى قَرَارٍ مَّكِينٍ
77:21 Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:22 إِلَىٰ قَدَرٍ مَّعْلُومٍ
77:22 Mpaka muda maalumu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:23 فَقَدَرْنَا فَنِعْمَ ٱلْقَـٰدِرُونَ
77:23 Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:24 وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
77:24 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:25 أَلَمْ نَجْعَلِ ٱلْأَرْضَ كِفَاتًا
77:25 Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:26 أَحْيَآءً وَأَمْوَٰتًا
77:26 Walio hai na maiti? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:27 وَجَعَلْنَا فِيهَا رَوَٰسِىَ شَـٰمِخَـٰتٍ وَأَسْقَيْنَـٰكُم مَّآءً فُرَاتًا
77:27 Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:28 وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
77:28 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:29 ٱنطَلِقُوٓا۟ إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
77:29 Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:30 ٱنطَلِقُوٓا۟ إِلَىٰ ظِلٍّ ذِى ثَلَـٰثِ شُعَبٍ
77:30 Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:31 لَّا ظَلِيلٍ وَلَا يُغْنِى مِنَ ٱللَّهَبِ
77:31 Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:32 إِنَّهَا تَرْمِى بِشَرَرٍ كَٱلْقَصْرِ
77:32 Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:33 كَأَنَّهُۥ جِمَـٰلَتٌ صُفْرٌ
77:33 Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:34 وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
77:34 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:35 هَـٰذَا يَوْمُ لَا يَنطِقُونَ
77:35 Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:36 وَلَا يُؤْذَنُ لَهُمْ فَيَعْتَذِرُونَ
77:36 Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:37 وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
77:37 Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:38 هَـٰذَا يَوْمُ ٱلْفَصْلِ ۖ جَمَعْنَـٰكُمْ وَٱلْأَوَّلِينَ
77:38 Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:39 فَإِن كَانَ لَكُمْ كَيْدٌ فَكِيدُونِ
77:39 Ikiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:40 وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
77:40 Ole wao siku hiyo hao walio kanusha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:41 إِنَّ ٱلْمُتَّقِينَ فِى ظِلَـٰلٍ وَعُيُونٍ
77:41 Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:42 وَفَوَٰكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ
77:42 Na matunda wanayo yapenda, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:43 كُلُوا۟ وَٱشْرَبُوا۟ هَنِيٓـًٔۢا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
77:43 Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:44 إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجْزِى ٱلْمُحْسِنِينَ
77:44 Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:45 وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
77:45 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:46 كُلُوا۟ وَتَمَتَّعُوا۟ قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجْرِمُونَ
77:46 Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:47 وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
77:47 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:48 وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱرْكَعُوا۟ لَا يَرْكَعُونَ
77:48 Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:49 وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ
77:49 Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

77:50 فَبِأَىِّ حَدِيثٍۭ بَعْدَهُۥ يُؤْمِنُونَ
77:50 Basi maneno gani baada ya haya watayaamini? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)