Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

78 An-Naba' ٱلنَّبَأ

< Previous   40 Āyah   The Tidings      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

78:1 عَمَّ يَتَسَآءَلُونَ
78:1 WANAULIZANA nini? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:2 عَنِ ٱلنَّبَإِ ٱلْعَظِيمِ
78:2 Ile khabari kuu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:3 ٱلَّذِى هُمْ فِيهِ مُخْتَلِفُونَ
78:3 Ambayo kwayo wanakhitalifiana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:4 كَلَّا سَيَعْلَمُونَ
78:4 La! Karibu watakuja jua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:5 ثُمَّ كَلَّا سَيَعْلَمُونَ
78:5 Tena la! Karibu watakuja jua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:6 أَلَمْ نَجْعَلِ ٱلْأَرْضَ مِهَـٰدًا
78:6 Kwani hatukuifanya ardhi kama tandiko? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:7 وَٱلْجِبَالَ أَوْتَادًا
78:7 Na milima kama vigingi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:8 وَخَلَقْنَـٰكُمْ أَزْوَٰجًا
78:8 Na tukakuumbeni kwa jozi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:9 وَجَعَلْنَا نَوْمَكُمْ سُبَاتًا
78:9 Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:10 وَجَعَلْنَا ٱلَّيْلَ لِبَاسًا
78:10 Na tukaufanya usiku ni nguo? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:11 وَجَعَلْنَا ٱلنَّهَارَ مَعَاشًا
78:11 Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:12 وَبَنَيْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعًا شِدَادًا
78:12 Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:13 وَجَعَلْنَا سِرَاجًا وَهَّاجًا
78:13 Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:14 وَأَنزَلْنَا مِنَ ٱلْمُعْصِرَٰتِ مَآءً ثَجَّاجًا
78:14 Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:15 لِّنُخْرِجَ بِهِۦ حَبًّا وَنَبَاتًا
78:15 Ili tutoe kwayo nafaka na mimea, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:16 وَجَنَّـٰتٍ أَلْفَافًا
78:16 Na mabustani yenye miti iliyo kamatana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:17 إِنَّ يَوْمَ ٱلْفَصْلِ كَانَ مِيقَـٰتًا
78:17 Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:18 يَوْمَ يُنفَخُ فِى ٱلصُّورِ فَتَأْتُونَ أَفْوَاجًا
78:18 Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:19 وَفُتِحَتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتْ أَبْوَٰبًا
78:19 Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:20 وَسُيِّرَتِ ٱلْجِبَالُ فَكَانَتْ سَرَابًا
78:20 Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:21 إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتْ مِرْصَادًا
78:21 Hakika Jahannamu inangojea! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:22 لِّلطَّـٰغِينَ مَـَٔابًا
78:22 Kwa walio asi ndio makaazi yao, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:23 لَّـٰبِثِينَ فِيهَآ أَحْقَابًا
78:23 Wakae humo karne baada ya karne, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:24 لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرْدًا وَلَا شَرَابًا
78:24 Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:25 إِلَّا حَمِيمًا وَغَسَّاقًا
78:25 Ila maji yamoto sana na usaha, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:26 جَزَآءً وِفَاقًا
78:26 Ndio jaza muwafaka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:27 إِنَّهُمْ كَانُوا۟ لَا يَرْجُونَ حِسَابًا
78:27 Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:28 وَكَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا كِذَّابًا
78:28 Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:29 وَكُلَّ شَىْءٍ أَحْصَيْنَـٰهُ كِتَـٰبًا
78:29 Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:30 فَذُوقُوا۟ فَلَن نَّزِيدَكُمْ إِلَّا عَذَابًا
78:30 Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:31 إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا
78:31 Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:32 حَدَآئِقَ وَأَعْنَـٰبًا
78:32 Mabustani na mizabibu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:33 وَكَوَاعِبَ أَتْرَابًا
78:33 Na wake walio lingana nao, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:34 وَكَأْسًا دِهَاقًا
78:34 Na bilauri zilizo jaa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:35 لَّا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا كِذَّٰبًا
78:35 Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo - - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:36 جَزَآءً مِّن رَّبِّكَ عَطَآءً حِسَابًا
78:36 Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:37 رَّبِّ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ٱلرَّحْمَـٰنِ ۖ لَا يَمْلِكُونَ مِنْهُ خِطَابًا
78:37 Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:38 يَوْمَ يَقُومُ ٱلرُّوحُ وَٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ صَفًّا ۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنْ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحْمَـٰنُ وَقَالَ صَوَابًا
78:38 Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:39 ذَٰلِكَ ٱلْيَوْمُ ٱلْحَقُّ ۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ مَـَٔابًا
78:39 Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

78:40 إِنَّآ أَنذَرْنَـٰكُمْ عَذَابًا قَرِيبًا يَوْمَ يَنظُرُ ٱلْمَرْءُ مَا قَدَّمَتْ يَدَاهُ وَيَقُولُ ٱلْكَافِرُ يَـٰلَيْتَنِى كُنتُ تُرَٰبًۢا
78:40 Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)