Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

96 Al-`Alaq ٱلْعَلَق

< Previous   19 Āyah   The Clot      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

96:1 ٱقْرَأْ بِٱسْمِ رَبِّكَ ٱلَّذِى خَلَقَ
96:1 Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:2 خَلَقَ ٱلْإِنسَـٰنَ مِنْ عَلَقٍ
96:2 Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:3 ٱقْرَأْ وَرَبُّكَ ٱلْأَكْرَمُ
96:3 Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:4 ٱلَّذِى عَلَّمَ بِٱلْقَلَمِ
96:4 Ambaye amefundisha kwa kalamu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:5 عَلَّمَ ٱلْإِنسَـٰنَ مَا لَمْ يَعْلَمْ
96:5 Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:6 كَلَّآ إِنَّ ٱلْإِنسَـٰنَ لَيَطْغَىٰٓ
96:6 Kwani! Hakika mtu bila ya shaka huwa jeuri - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:7 أَن رَّءَاهُ ٱسْتَغْنَىٰٓ
96:7 Akijiona katajirika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:8 إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجْعَىٰٓ
96:8 Hakika kwa Mola wako Mlezi ndio marejeo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:9 أَرَءَيْتَ ٱلَّذِى يَنْهَىٰ
96:9 Umemwona yule anaye mkataza - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:10 عَبْدًا إِذَا صَلَّىٰٓ
96:10 Mja anapo sali? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:11 أَرَءَيْتَ إِن كَانَ عَلَى ٱلْهُدَىٰٓ
96:11 Umeona kama yeye yuko juu ya uwongofu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:12 أَوْ أَمَرَ بِٱلتَّقْوَىٰٓ
96:12 Au anaamrisha uchamngu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:13 أَرَءَيْتَ إِن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰٓ
96:13 Umeona kama yeye akikanusha na anarudi nyuma? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:14 أَلَمْ يَعْلَم بِأَنَّ ٱللَّهَ يَرَىٰ
96:14 Hajui ya kwamba Mwenyezi Mungu anaona? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:15 كَلَّا لَئِن لَّمْ يَنتَهِ لَنَسْفَعًۢا بِٱلنَّاصِيَةِ
96:15 Kwani! Kama haachi, tutamkokota kwa shungi la nywele! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:16 نَاصِيَةٍ كَـٰذِبَةٍ خَاطِئَةٍ
96:16 Shungi la uwongo, lenye makosa! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:17 فَلْيَدْعُ نَادِيَهُۥ
96:17 Basi na awaite wenzake! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:18 سَنَدْعُ ٱلزَّبَانِيَةَ
96:18 Nasi tutawaita Mazabania! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

96:19 كَلَّا لَا تُطِعْهُ وَٱسْجُدْ وَٱقْتَرِب ۩
96:19 Hasha! Usimt'ii! Nawe sujudu na ujongee! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)