Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

80 `Abasa عَبَسَ

< Previous   42 Āyah   He Frowned      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

80:1 عَبَسَ وَتَوَلَّىٰٓ
80:1 Alikunja kipaji na akageuka, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:2 أَن جَآءَهُ ٱلْأَعْمَىٰ
80:2 Kwa sababu alimjia kipofu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:3 وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُۥ يَزَّكَّىٰٓ
80:3 Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:4 أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ ٱلذِّكْرَىٰٓ
80:4 Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:5 أَمَّا مَنِ ٱسْتَغْنَىٰ
80:5 Ama ajionaye hana haja, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:6 فَأَنتَ لَهُۥ تَصَدَّىٰ
80:6 Wewe ndio unamshughulikia? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:7 وَمَا عَلَيْكَ أَلَّا يَزَّكَّىٰ
80:7 Na si juu yako kama hakutakasika. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:8 وَأَمَّا مَن جَآءَكَ يَسْعَىٰ
80:8 Ama anaye kujia kwa juhudi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:9 وَهُوَ يَخْشَىٰ
80:9 Naye anaogopa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:10 فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّىٰ
80:10 Ndio wewe unampuuza? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:11 كَلَّآ إِنَّهَا تَذْكِرَةٌ
80:11 Sivyo hivyo! Huku ni kukumbushana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:12 فَمَن شَآءَ ذَكَرَهُۥ
80:12 Basi anaye penda akumbuke. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:13 فِى صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ
80:13 Yamo katika kurasa zilizo hishimiwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:14 مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍۭ
80:14 Zilizo inuliwa, zilizo takaswa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:15 بِأَيْدِى سَفَرَةٍ
80:15 Zimo mikononi mwa Malaika waandishi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:16 كِرَامٍۭ بَرَرَةٍ
80:16 Watukufu, wema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:17 قُتِلَ ٱلْإِنسَـٰنُ مَآ أَكْفَرَهُۥ
80:17 Ameangamia mwanaadamu! Nini kinacho mkufurisha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:18 مِنْ أَىِّ شَىْءٍ خَلَقَهُۥ
80:18 Kwa kitu gani amemuumba? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:19 مِن نُّطْفَةٍ خَلَقَهُۥ فَقَدَّرَهُۥ
80:19 Kwa tone la manii, akamuumba na akamkadiria. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:20 ثُمَّ ٱلسَّبِيلَ يَسَّرَهُۥ
80:20 Kisha akamsahilishia njia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:21 ثُمَّ أَمَاتَهُۥ فَأَقْبَرَهُۥ
80:21 Kisha akamfisha, akamtia kaburini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:22 ثُمَّ إِذَا شَآءَ أَنشَرَهُۥ
80:22 Kisha apendapo atamfufua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:23 كَلَّا لَمَّا يَقْضِ مَآ أَمَرَهُۥ
80:23 La! Hajamaliza aliyo muamuru. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:24 فَلْيَنظُرِ ٱلْإِنسَـٰنُ إِلَىٰ طَعَامِهِۦٓ
80:24 Hebu mtu na atazame chakula chake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:25 أَنَّا صَبَبْنَا ٱلْمَآءَ صَبًّا
80:25 Hakika Sisi tumemimina maji kwa nguvu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:26 ثُمَّ شَقَقْنَا ٱلْأَرْضَ شَقًّا
80:26 Tena tukaipasua pasua ardhi kwa nguvu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:27 فَأَنۢبَتْنَا فِيهَا حَبًّا
80:27 Kisha tukaotesha humo nafaka, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:28 وَعِنَبًا وَقَضْبًا
80:28 Na zabibu, na mimea ya majani, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:29 وَزَيْتُونًا وَنَخْلًا
80:29 Na mizaituni, na mitende, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:30 وَحَدَآئِقَ غُلْبًا
80:30 Na bustani zenye miti iliyo songana baraabara, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:31 وَفَـٰكِهَةً وَأَبًّا
80:31 Na matunda, na malisho ya wanyama; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:32 مَّتَـٰعًا لَّكُمْ وَلِأَنْعَـٰمِكُمْ
80:32 Kwa manufaa yenu na mifugo yenu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:33 فَإِذَا جَآءَتِ ٱلصَّآخَّةُ
80:33 Basi utakapo kuja ukelele, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:34 يَوْمَ يَفِرُّ ٱلْمَرْءُ مِنْ أَخِيهِ
80:34 Siku ambayo mtu atamkimbia nduguye, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:35 وَأُمِّهِۦ وَأَبِيهِ
80:35 Na mamaye na babaye, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:36 وَصَـٰحِبَتِهِۦ وَبَنِيهِ
80:36 Na mkewe na wanawe - - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:37 لِكُلِّ ٱمْرِئٍ مِّنْهُمْ يَوْمَئِذٍ شَأْنٌ يُغْنِيهِ
80:37 Kila mtu miongoni mwao siku hiyo atakuwa na lake la kumtosha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:38 وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ مُّسْفِرَةٌ
80:38 Siku hiyo ziko nyuso zitazo nawiri, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:39 ضَاحِكَةٌ مُّسْتَبْشِرَةٌ
80:39 Zitacheka, zitachangamka; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:40 وَوُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ عَلَيْهَا غَبَرَةٌ
80:40 Na nyuso siku hiyo zitakuwa na mavumbi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:41 تَرْهَقُهَا قَتَرَةٌ
80:41 Giza totoro litazifunika, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

80:42 أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْكَفَرَةُ ٱلْفَجَرَةُ
80:42 Hao ndio makafiri watenda maovu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)