Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

56 Al-Wāqi`ah ٱلْوَاقِعَة

< Previous   96 Āyah   The Inevitable      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

56:1 إِذَا وَقَعَتِ ٱلْوَاقِعَةُ
56:1 Litakapo tukia hilo Tukio - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:2 لَيْسَ لِوَقْعَتِهَا كَاذِبَةٌ
56:2 Hapana cha kukanusha kutukia kwake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:3 خَافِضَةٌ رَّافِعَةٌ
56:3 Literemshalo linyanyualo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:4 إِذَا رُجَّتِ ٱلْأَرْضُ رَجًّا
56:4 Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:5 وَبُسَّتِ ٱلْجِبَالُ بَسًّا
56:5 Na milima itapo sagwasagwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:6 فَكَانَتْ هَبَآءً مُّنۢبَثًّا
56:6 Iwe mavumbi yanayo peperushwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:7 وَكُنتُمْ أَزْوَٰجًا ثَلَـٰثَةً
56:7 Na nyinyi mtakuwa namna tatu:- - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:8 فَأَصْحَـٰبُ ٱلْمَيْمَنَةِ مَآ أَصْحَـٰبُ ٱلْمَيْمَنَةِ
56:8 Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:9 وَأَصْحَـٰبُ ٱلْمَشْـَٔمَةِ مَآ أَصْحَـٰبُ ٱلْمَشْـَٔمَةِ
56:9 Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:10 وَٱلسَّـٰبِقُونَ ٱلسَّـٰبِقُونَ
56:10 Na wa mbele watakuwa mbele. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:11 أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلْمُقَرَّبُونَ
56:11 Hao ndio watakao karibishwa - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:12 فِى جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ
56:12 Katika Bustani zenye neema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:13 ثُلَّةٌ مِّنَ ٱلْأَوَّلِينَ
56:13 Fungu kubwa katika wa mwanzo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:14 وَقَلِيلٌ مِّنَ ٱلْـَٔاخِرِينَ
56:14 Na wachache katika wa mwisho. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:15 عَلَىٰ سُرُرٍ مَّوْضُونَةٍ
56:15 Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:16 مُّتَّكِـِٔينَ عَلَيْهَا مُتَقَـٰبِلِينَ
56:16 Wakiviegemea wakielekeana. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:17 يَطُوفُ عَلَيْهِمْ وِلْدَٰنٌ مُّخَلَّدُونَ
56:17 Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:18 بِأَكْوَابٍ وَأَبَارِيقَ وَكَأْسٍ مِّن مَّعِينٍ
56:18 Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:19 لَّا يُصَدَّعُونَ عَنْهَا وَلَا يُنزِفُونَ
56:19 Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:20 وَفَـٰكِهَةٍ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ
56:20 Na matunda wayapendayo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:21 وَلَحْمِ طَيْرٍ مِّمَّا يَشْتَهُونَ
56:21 Na nyama za ndege kama wanavyo tamani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:22 وَحُورٌ عِينٌ
56:22 Na Mahurulaini, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:23 كَأَمْثَـٰلِ ٱللُّؤْلُؤِ ٱلْمَكْنُونِ
56:23 Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:24 جَزَآءًۢ بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ
56:24 Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:25 لَا يَسْمَعُونَ فِيهَا لَغْوًا وَلَا تَأْثِيمًا
56:25 Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:26 إِلَّا قِيلًا سَلَـٰمًا سَلَـٰمًا
56:26 Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:27 وَأَصْحَـٰبُ ٱلْيَمِينِ مَآ أَصْحَـٰبُ ٱلْيَمِينِ
56:27 Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:28 فِى سِدْرٍ مَّخْضُودٍ
56:28 Katika mikunazi isiyo na miba, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:29 وَطَلْحٍ مَّنضُودٍ
56:29 Na migomba iliyo pangiliwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:30 وَظِلٍّ مَّمْدُودٍ
56:30 Na kivuli kilicho tanda, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:31 وَمَآءٍ مَّسْكُوبٍ
56:31 Na maji yanayo miminika, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:32 وَفَـٰكِهَةٍ كَثِيرَةٍ
56:32 Na matunda mengi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:33 لَّا مَقْطُوعَةٍ وَلَا مَمْنُوعَةٍ
56:33 Hayatindikii wala hayakatazwi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:34 وَفُرُشٍ مَّرْفُوعَةٍ
56:34 Na matandiko yaliyo nyanyuliwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:35 إِنَّآ أَنشَأْنَـٰهُنَّ إِنشَآءً
56:35 Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:36 فَجَعَلْنَـٰهُنَّ أَبْكَارًا
56:36 Na tutawafanya vijana, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:37 عُرُبًا أَتْرَابًا
56:37 Wanapendana na waume zao, hirimu moja. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:38 لِّأَصْحَـٰبِ ٱلْيَمِينِ
56:38 Kwa ajili ya watu wa kuliani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:39 ثُلَّةٌ مِّنَ ٱلْأَوَّلِينَ
56:39 Fungu kubwa katika wa mwanzo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:40 وَثُلَّةٌ مِّنَ ٱلْـَٔاخِرِينَ
56:40 Na fungu kubwa katika wa mwisho. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:41 وَأَصْحَـٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصْحَـٰبُ ٱلشِّمَالِ
56:41 Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:42 فِى سَمُومٍ وَحَمِيمٍ
56:42 Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:43 وَظِلٍّ مِّن يَحْمُومٍ
56:43 Na kivuli cha moshi mweusi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:44 لَّا بَارِدٍ وَلَا كَرِيمٍ
56:44 Si cha kuburudisha wala kustarehesha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:45 إِنَّهُمْ كَانُوا۟ قَبْلَ ذَٰلِكَ مُتْرَفِينَ
56:45 Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:46 وَكَانُوا۟ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلْحِنثِ ٱلْعَظِيمِ
56:46 Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:47 وَكَانُوا۟ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ
56:47 Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:48 أَوَءَابَآؤُنَا ٱلْأَوَّلُونَ
56:48 Au baba zetu wa zamani? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:49 قُلْ إِنَّ ٱلْأَوَّلِينَ وَٱلْـَٔاخِرِينَ
56:49 Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:50 لَمَجْمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَـٰتِ يَوْمٍ مَّعْلُومٍ
56:50 Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:51 ثُمَّ إِنَّكُمْ أَيُّهَا ٱلضَّآلُّونَ ٱلْمُكَذِّبُونَ
56:51 Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:52 لَـَٔاكِلُونَ مِن شَجَرٍ مِّن زَقُّومٍ
56:52 Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:53 فَمَالِـُٔونَ مِنْهَا ٱلْبُطُونَ
56:53 Na kwa mti huo mtajaza matumbo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:54 فَشَـٰرِبُونَ عَلَيْهِ مِنَ ٱلْحَمِيمِ
56:54 Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:55 فَشَـٰرِبُونَ شُرْبَ ٱلْهِيمِ
56:55 Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:56 هَـٰذَا نُزُلُهُمْ يَوْمَ ٱلدِّينِ
56:56 Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:57 نَحْنُ خَلَقْنَـٰكُمْ فَلَوْلَا تُصَدِّقُونَ
56:57 Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:58 أَفَرَءَيْتُم مَّا تُمْنُونَ
56:58 Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:59 ءَأَنتُمْ تَخْلُقُونَهُۥٓ أَمْ نَحْنُ ٱلْخَـٰلِقُونَ
56:59 Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:60 نَحْنُ قَدَّرْنَا بَيْنَكُمُ ٱلْمَوْتَ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ
56:60 Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:61 عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ أَمْثَـٰلَكُمْ وَنُنشِئَكُمْ فِى مَا لَا تَعْلَمُونَ
56:61 Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:62 وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ ٱلنَّشْأَةَ ٱلْأُولَىٰ فَلَوْلَا تَذَكَّرُونَ
56:62 Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:63 أَفَرَءَيْتُم مَّا تَحْرُثُونَ
56:63 Je! Mnaona makulima mnayo yapanda? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:64 ءَأَنتُمْ تَزْرَعُونَهُۥٓ أَمْ نَحْنُ ٱلزَّٰرِعُونَ
56:64 Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:65 لَوْ نَشَآءُ لَجَعَلْنَـٰهُ حُطَـٰمًا فَظَلْتُمْ تَفَكَّهُونَ
56:65 Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:66 إِنَّا لَمُغْرَمُونَ
56:66 Mkisema: Hakika sisi tumegharimika; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:67 بَلْ نَحْنُ مَحْرُومُونَ
56:67 Bali sisi tumenyimwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:68 أَفَرَءَيْتُمُ ٱلْمَآءَ ٱلَّذِى تَشْرَبُونَ
56:68 Je! Mnayaona maji mnayo yanywa? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:69 ءَأَنتُمْ أَنزَلْتُمُوهُ مِنَ ٱلْمُزْنِ أَمْ نَحْنُ ٱلْمُنزِلُونَ
56:69 Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:70 لَوْ نَشَآءُ جَعَلْنَـٰهُ أُجَاجًا فَلَوْلَا تَشْكُرُونَ
56:70 Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:71 أَفَرَءَيْتُمُ ٱلنَّارَ ٱلَّتِى تُورُونَ
56:71 Je! Mnauona moto mnao uwasha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:72 ءَأَنتُمْ أَنشَأْتُمْ شَجَرَتَهَآ أَمْ نَحْنُ ٱلْمُنشِـُٔونَ
56:72 Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:73 نَحْنُ جَعَلْنَـٰهَا تَذْكِرَةً وَمَتَـٰعًا لِّلْمُقْوِينَ
56:73 Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:74 فَسَبِّحْ بِٱسْمِ رَبِّكَ ٱلْعَظِيمِ
56:74 Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:75 ۞ فَلَآ أُقْسِمُ بِمَوَٰقِعِ ٱلنُّجُومِ
56:75 Basi naapa kwa maanguko ya nyota, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:76 وَإِنَّهُۥ لَقَسَمٌ لَّوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ
56:76 Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:77 إِنَّهُۥ لَقُرْءَانٌ كَرِيمٌ
56:77 Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:78 فِى كِتَـٰبٍ مَّكْنُونٍ
56:78 Katika Kitabu kilicho hifadhiwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:79 لَّا يَمَسُّهُۥٓ إِلَّا ٱلْمُطَهَّرُونَ
56:79 Hapana akigusaye ila walio takaswa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:80 تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ
56:80 Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:81 أَفَبِهَـٰذَا ٱلْحَدِيثِ أَنتُم مُّدْهِنُونَ
56:81 Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:82 وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ
56:82 Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:83 فَلَوْلَآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلْحُلْقُومَ
56:83 Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:84 وَأَنتُمْ حِينَئِذٍ تَنظُرُونَ
56:84 Na nyinyi wakati huo mnatazama! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:85 وَنَحْنُ أَقْرَبُ إِلَيْهِ مِنكُمْ وَلَـٰكِن لَّا تُبْصِرُونَ
56:85 Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:86 فَلَوْلَآ إِن كُنتُمْ غَيْرَ مَدِينِينَ
56:86 Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:87 تَرْجِعُونَهَآ إِن كُنتُمْ صَـٰدِقِينَ
56:87 Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:88 فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلْمُقَرَّبِينَ
56:88 Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:89 فَرَوْحٌ وَرَيْحَانٌ وَجَنَّتُ نَعِيمٍ
56:89 Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:90 وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنْ أَصْحَـٰبِ ٱلْيَمِينِ
56:90 Na akiwa katika watu wa upande wa kulia, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:91 فَسَلَـٰمٌ لَّكَ مِنْ أَصْحَـٰبِ ٱلْيَمِينِ
56:91 Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:92 وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلْمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّينَ
56:92 Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:93 فَنُزُلٌ مِّنْ حَمِيمٍ
56:93 Basi karamu yake ni maji yanayo chemka, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:94 وَتَصْلِيَةُ جَحِيمٍ
56:94 Na kutiwa Motoni. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:95 إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ حَقُّ ٱلْيَقِينِ
56:95 Hakika hii ndiyo haki yenye yakini. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

56:96 فَسَبِّحْ بِٱسْمِ رَبِّكَ ٱلْعَظِيمِ
56:96 Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)