Selected

Original Text
Ali Muhsin Al-Barwani

Available Translations

89 Al-Fajr ٱلْفَجْر

< Previous   30 Āyah   The Dawn      Next >  

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
In the name of Allah, Most Gracious, Most Merciful.

89:1 وَٱلْفَجْرِ
89:1 Naapa kwa alfajiri, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:2 وَلَيَالٍ عَشْرٍ
89:2 Na kwa masiku kumi, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:3 وَٱلشَّفْعِ وَٱلْوَتْرِ
89:3 Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:4 وَٱلَّيْلِ إِذَا يَسْرِ
89:4 Na kwa usiku unapo pita, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:5 هَلْ فِى ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِى حِجْرٍ
89:5 Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:6 أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ
89:6 Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:7 إِرَمَ ذَاتِ ٱلْعِمَادِ
89:7 Wa Iram, wenye majumba marefu? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:8 ٱلَّتِى لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِى ٱلْبِلَـٰدِ
89:8 Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:9 وَثَمُودَ ٱلَّذِينَ جَابُوا۟ ٱلصَّخْرَ بِٱلْوَادِ
89:9 Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:10 وَفِرْعَوْنَ ذِى ٱلْأَوْتَادِ
89:10 Na Firauni mwenye vigingi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:11 ٱلَّذِينَ طَغَوْا۟ فِى ٱلْبِلَـٰدِ
89:11 Ambao walifanya jeuri katika nchi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:12 فَأَكْثَرُوا۟ فِيهَا ٱلْفَسَادَ
89:12 Wakakithirisha humo ufisadi? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:13 فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ
89:13 Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:14 إِنَّ رَبَّكَ لَبِٱلْمِرْصَادِ
89:14 Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:15 فَأَمَّا ٱلْإِنسَـٰنُ إِذَا مَا ٱبْتَلَىٰهُ رَبُّهُۥ فَأَكْرَمَهُۥ وَنَعَّمَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّىٓ أَكْرَمَنِ
89:15 Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:16 وَأَمَّآ إِذَا مَا ٱبْتَلَىٰهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّىٓ أَهَـٰنَنِ
89:16 Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:17 كَلَّا ۖ بَل لَّا تُكْرِمُونَ ٱلْيَتِيمَ
89:17 Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:18 وَلَا تَحَـٰٓضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلْمِسْكِينِ
89:18 Wala hamhimizani kulisha masikini; - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:19 وَتَأْكُلُونَ ٱلتُّرَاثَ أَكْلًا لَّمًّا
89:19 Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:20 وَتُحِبُّونَ ٱلْمَالَ حُبًّا جَمًّا
89:20 Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:21 كَلَّآ إِذَا دُكَّتِ ٱلْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا
89:21 Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:22 وَجَآءَ رَبُّكَ وَٱلْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا
89:22 Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:23 وَجِا۟ىٓءَ يَوْمَئِذٍۭ بِجَهَنَّمَ ۚ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ ٱلْإِنسَـٰنُ وَأَنَّىٰ لَهُ ٱلذِّكْرَىٰ
89:23 Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini? - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:24 يَقُولُ يَـٰلَيْتَنِى قَدَّمْتُ لِحَيَاتِى
89:24 Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:25 فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُۥٓ أَحَدٌ
89:25 Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:26 وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُۥٓ أَحَدٌ
89:26 Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:27 يَـٰٓأَيَّتُهَا ٱلنَّفْسُ ٱلْمُطْمَئِنَّةُ
89:27 Ewe nafsi iliyo tua! - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:28 ٱرْجِعِىٓ إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً
89:28 Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:29 فَٱدْخُلِى فِى عِبَـٰدِى
89:29 Basi ingia miongoni mwa waja wangu, - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)

89:30 وَٱدْخُلِى جَنَّتِى
89:30 Na ingia katika Pepo yangu. - Ali Muhsin Al-Barwani (Swahili)